UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU.

 Kijana Lawrent Lawrian, akiwa na uvimbe wa ajabu kichwani mwake.
Lawrent Lawrian, 42 (pichani), ni mkazi wa Kijiji cha Nyakisogo, Wilaya ya Biharamlo, mkoani Kagera, amekuwa mwenye huzuni na kukosa raha kwa muda wa miaka 35 kutokana na gonjwa la ajabu linalomtesa ambalo limemsababishia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutoendelea na masomo.
 Gonjwa hilo la ajabu ni uvimbe kama nundu kichwani wenye uzito wa kilo 3, ulimuanza akiwa darasa la kwanza.Akielezea zaidi kwa njia ya simu hivi karibuni Lawrent alisema: “Gonjwa hili lilianza kama kauvimbe nikiwa na umri wa miaka saba, wakati huo nilikuwa na wazazi wote na ilipofika mwaka 1992 baba akafariki dunia. “Nikabakia na mama tukawa tunaishi kwa kutegemea kilimo cha kawaida, nilikuwa nikienda shule lakini ilifikia hatua nilishindwa kutokana na maumivu na manyanyaso. “Darasa la saba nilimaliza kwa tabu sana, kwani wanafunzi wenzangu walikuwa wakinicheka na kunitenga, licha ya kuadhibiwa na walimu lakini hawakuacha tabia yao.“Kutokana na hali hiyo, nilishindwa kuendelea na masomo kwani nilikuwa nikifungiwa ndani ili kunipunguzia kero toka kwa wenzangu.SOMA ZAIDI>>>

Comments

Popular posts from this blog