TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA NISHATI KWA NCHI ZA AFRIKA

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea wakati wa mkutano wa Mawaziri wanaohusika na masuala ya Nishati ambapo aliwatangazia wajumbe hao kwamba Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Bara la Afrika kuhusu Nishati Endelevu katika muda utaopangwa na Umoja wa Mataifa.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa siku tatu wa Nishati Endelevu kwa Wote ( SE4ALL) ulioandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Eng. Yahya Samamba Katibu wa Waziri na Eng. Styden Rwebangila
Watanzania wengine ambao ni sehumu ya Ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Bi. Venosa Ngow ( TPDC) Eng. Leonard Masanja kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Eng Jones fredrick Olutu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeelezea utayari wake wa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bara la Afrika kuhushu Nishati Endelevu kwa wote.

Ahadi hiyo imetolewa siku ya Ijumaa, na Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) mwishoni wa mkutano wa siku tatu , uliojadili kwa kina upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote. Mkutano huu uliojumuisha wadau wa kada mbalimbali uliandaliwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo pia palifanyika uzinduzi wa mwongo wa nishati endelevu kwa wote unaoanza 2014 hadi 2024.

“ Ninapenda kutaarifu kwamba, nimezungumza na Rais wangu, Tanzania iko tayari kuwa mwenyejiji wa mkutano wa nchi za Afrika kuhusu nishati endelevu. Tutakuwa wenyeji wa mkutano huo pale Umoja wa Mataifa utakapokuwa tayari”. akasema Waziri Muhongo. Kauli iliyopokelewa vema na waandaji wa mkutano huo. 

Waziri Muhongo ambaye ameshiriki kikamilifu mijadala mbalimbali tangu mwanzo wa mkutano hadi mwisho, alisema Tanzania na kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi hasa za Afrika, Nishati Endelevu ni muhimu katika utekelezaji na ufanikishaji wa Maendeleo Endelevu badaa ya mwaka 2015.

Akasisitiza kuwa katika utekelezaji wa mpango wa nishati mbadala kwa wote, Afrika inapashwa kupewa kipaumbele cha pekee.

Katika siku hii ya tatu na ya mwisho ya mkutano huu, Mawaziri walioziwakilisha nchi zao, walipata fursa ya kubadilishana mawazo, kuelezea uzoefu wao, kutoa maoni yao na halikadhalika kupendekeza nini cha kufanya ili hatimaye watu wengi zaidi hususani katika nchi zinazoendelea waweze kupata huduma hii ya nishati endelevu.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu 1.3 bilioni duniani kote hawana huduma ya umeme na zaidi wa 2.6 bilioni wanatumia nishati asilia kwa kupikia na kupata joto. Matumizi ya nishati asilia yanasababisha watu 4.3 milioni kufariki kila mwaka kabla ya wakati wao huku wengi kati yao wakiwa ni wanawake na watoto kutokana na uvutaji wa moshi.

Waziri Muhongo ambaye ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu akiwamo Muhandisi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini. Amesisitiza pia uhusiamo kati ya nishati na elimu kwa kile alichosema ili mwanafunzi aweze kujiandaa au kujisomea vizuri anahitaji nishati ambayo ni endelevu na yenye uhakikia.

“ Hii itakuwa mara yangu ya nne kutoa maoni na mchango wangu na kwa sababu hiyo nisingepeda kutumia muda mwingi na pengine kurudia kile ambacho nimeshakisema huko nyuma. Nisisitize kwamba tunapozungumzia mpango wa nishati endelevu kwa wote basin chi za afrika zinatakuwa kupewa kipaumbele cha pekee, vile vile suala la uwepo wa nishati endelevu lina uhusiano mkubwa na utekelezaji wa maendeleo endelevu baada ya 2015.

Akasisitiza kuwa Tanzania imejipanga vema katika kuhakikisha kwamba wananchi wake wanapatiwa huduma hiyo muhi

Comments

Popular posts from this blog