MISS IRINGA KUFANYIKA JUNI 20

Baadhi ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill iliyoko mkoani Iringa. 

Na Denis Mlowe,Iringa
 
HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.
 
Waandaji wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.
 
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana Mkurugenz wa kampuni hiyo, Victor Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
 
Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
 
Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
 
“Kwa kweli baada ya mratibu wa kwanza kukimbia kutokana na gharama za uandaaji niliamua kuchukua jukumu hilo kulikomboa shindano hilo lifanyike na warembo wengi wamejitokeza kushiriki miss iringa” alisema Chakudika.
 
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa. Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.

Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.

Comments

Popular posts from this blog