Kiongozi wa kiislamu aliyeuwawa Kenya.

mohamed
Kiongozi wa wahubiri wa kiislam nchini Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa mwambao wa Mombasa, yakiwa ni mauaji ya hivi karibuni.Sheikh Mohammed Idris, mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kenya, ameuawa karibu na msikiti uliopo karibu na nyumbani kwake na kundi la vijana wenye silaha.Taatifa zinasema kuwa hapo awali amekuwa akipata vitisho kutoka kwa baadhi vijana wa kiislam na kuhofia maisha yake.Waislam kadhaa maarufu wenye msimamo mkali wamekua wakiuawa kwa kupigwa risasi katika hali isiyoelezeka miaka ya hivi karibuni.
Wengine walikuwa wakituhumiwa kuwa ni viungo wa kundi la kiislam la Al-Shabab la nchini Somalia ambapo wafuasi wao wamekua wakiishutumu serikali kuhusika na mauaji hayo, shutuma ambazo mamlaka imezikataa.Hivi karibuni Idris, alilitaka jeshi la polisi kupambana na vikundi vyenye muelekeo wa kijeshi katika msikiti wake, na kupelekea wengine kumuona kama msaliti.

Comments

Popular posts from this blog