AVEVA NDIYE RAIS MPYA SIMBA SC...ASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA

Amin Bakhresa akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Simba SC.
Evance Aveva akishukuru baada ya kutangazwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba na kuchukua mikoba ya Ismail Aden Rage, aliyemaliza muda wake wa miaka minne.Rais mpya wa Simba, Aveva akipongeza Bakhresa kwa kazi nzuri ya kusimamia shughuli nzima ya uchaguzi, ambao ulifanyika pasipo bugudha yoyote ile katika Bwalo la Polisi Oysterbay jana
 MIKAKATI IMEANZA! Rais mpya wa Simba Aveva (mwenye suti, kushoto), akisalimiana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga huku Makamu Katibu Mkuu Phillip Stanley (mwenye shati jekundu) akiwasikiliza mipango yao.
  Rais Aveva, akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti uongozi uliomaliza muda wake, Joseph Itang'are 'Mzee Kines' baada ya shughuli nzima ya uchaguzi kumalizika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)

Comments

Popular posts from this blog