MBINU TANO(5) ZA KUISHI NA WAFANYAKAZI WENZAKO AMBAO NI WAKOROFI




Huyu mtu siku zote ni mkorofi na mwenye kukusababishia hasira. Hata ukiongea naye kwa utaratibu lazima alete maudhi, anakusababishia kazi uione mbaya kila unapomwona. Unahitaji mbinu za kuishi naye.
 
1. Utambue ya kuwa sio wewe peke yako
Unaweza kusema kwamba huyu mtu ana visa na wewe tu, mara nyingi watu wa namna hii ni kwa jinsi tu ya tabia zao na namna walivyokuzwa. Jitahidi kwa kadri uwezavyo kutotilia maanani wanachokiongea ili usiingie kwenye ugomvi bila sababu. Wengine huwa hawajui kwamba wanakera wenzao kwa namna ambavyo wanafanya au kuongea, wao hupenda namna wanavyojisikia kila wanachofanya au kusema ndio furaha yao.

2. Jiepushe nao
Punguza au ujiepushe kukutana nao mara kwa mara ili kupunguza kero. Hata kama watafika ofisini kwako, onyesha uko kikazi zaidi kuliko utani na mambo yasiyo ya msingi. Kama kuna jambo wanauliza waombe kukutumia barua pepe au kuacha ujumbe kwenye dawati lako la kazi. Unapopunguza kukutana nao mara kwa mara unaboresha namna unavyowasiliana nao na kupunguza kero.

3. Gundua kero hasa ni nini?
Huwezi kujua kwa urahisi huyu mtu au watu hawa huwa wanakera kwa kitu gani, jaribu kujua tabia zao na nini hasa wanakukera. Inawezekana huyu mtu au hao watu hawajui majukumu yao ya kazi vizuri na wamfuate nani, hivyo hujikuta wakimfuata kila mtu.utakapo gundua kero ya huyo mtu ndipo utapata urahisi wa kushughulikia kero hiyo.

4. Fanya Maboresho
Unaweza kugundua kwamba umepunguza kuhusiana naye kwa namna mbalimbali ila bado ukikutana naye ni kero. Inabidi uweke mpango wa kuboresha mambo, jitizame mwenyewe kama unaweza badirika katika mambo fulani ili uweze kumsaidia na yeye. Badilisha namna unavyomjibu, punguza jazba na utulie kila unapokutana naye au kuwa na mazungumzo naye. Je unafanya nini mtu huyu kufanya anachokifanya kila siku? Unaweza kubadirika namna unavyohusiana naye lakini huwezi kubadilisha mwitikio wao, dhamiria kusaidia kila unapokutana na huyo mtu.

5. Husiana naye kitaaluma zaidi
Haijalishi ni namna gani mtu huyu atakuwa akikufanyia, pambana naye kitaaluma zaidi kama bado ni mtata au ana kera. Inamaanisha usilaumu, wala kumsema hakikisha akija kwako mnaongelea kazi na baada ya hapo kila mtu anashika njia yake. Mwitikio wako unatakiwa uwe kwenye tabia na sio hulka yake. Kila kitu kinachofanyika kitizame kwenye mlengo wa kikazi au kibiashara na matokeo yake yanakuwaje.
Njia ya kuboresha na kukua kitaaluma haitakuwa rahisi na iliyonyooka. Inawezekana tukafurahi tunapoajiliwa, tukafurahia kazi, watu na hata tunapopongezwa na kupandishwa vyeo. Utakutana na watu wanaoudhi , wakorofi na hata wagomvi wakati mwingine utahitajika kufanya kitu cha ziada kuboresha maisha yako kazini na kwa watu wengine.
USISAHAU KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK ILI KUPATA HABARI ZAIDI

Comments

Popular posts from this blog