AFYA: DALILI ZA KUSAMBAA KWA KANSA YA MATITI

 leo tunaelezea dalili za kusambaa kwa saratani hii mwilini.Kitendo cha kansa kusambaa mwilini kupitia mkondo wa damu na limfu huitwa metastasis.  

Kusambaa kwa saratani hadi kwenye viungo na tishu muhimu kama vile ubongo, ini, mifupa au mapafu  bado kunaufanya ugonjwa huo kuwa hatari.
Dalili za saratani kusambaa mwilini ni maumivu ya mifupa, maumivu kwenye titi, vidonda kwenye ngozi, kuvimba mkono karibu na eneo la saratani na kupungua uzito.


Pia mgonjwa huweza kuhisi dalili tofauti kwa kutegemea saratani ya matiti imesambaa kwenye kiungo gani mwilini.
Kwa mfano saratani ya matiti iliyosambaa kwenye ini inaweza kusababisha mwili kuwa manjano, kuongezea kiwango cha enzymes katika ini, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika.


 Takwimu zinaonyesha kuwa, asilimia 70 ya wagonjwa wenye kusumbuliwa na saratani ya matiti, hupatwa na saratani iliyosambaa kwenye mifupa.
Hii ni katika hali ambayo asilimia 10 huweza kupata saratani ya matiti iliyosambaa kwenye ubongo.
 Kwa bahati mbaya tiba nyingi za kansa ya matiti hushindwa kupenya kwenye ubongo kwa hivyo huwa kuna uwezekano ugonjwa huo ukadhihirika tena katika mfumo wa kati wa fahamu.
USHAURI
Licha ya ugonjwa wa kansa ya matiti kuwa hatari mno kwa maisha yetu hasa wanawake, lakini aina hii ya saratani inaweza kutibiwa, iwapo tu tutaweza kuigundua mapema kwa kuwa na mazoea ya kuchunguza dalili za kansa ya matiti katika miili yetu.

Comments

Popular posts from this blog