TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI


Tatizo la uchafu ukeni
Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua
wanawake wengi, tatizo la kutokwa na
uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za
siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa
na majimaji yenye rangi nyeupe au ya
njano, 



ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo
endapo majimaji hayo siyo mazito sana na
wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo
majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au kahawia,
yanatoa harufu kali na yanawasha, basi
hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao
Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu
za siri ni njia inayowezesha viungo vya
uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa
uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya
damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga
viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya
bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa.
Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na
huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia
huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia
kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na
huzalishwa kwenye tezi za Bartholin
(Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo
ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha
gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye
mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila
siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au
kupungua kutegemeana na mzunguko wa
hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na
unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na
kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye
rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na
huwatoka wanawake wote hususan baada
ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu huo
Kuna sababu nyingi ambazo husababisha
mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya
kawaida kutoka kwenye sehemu zake za
siri. Maambukizi ya bacteria
wanaosababisha magonjwa kama
Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au
uambukizo wa bacteria Candida albicans,
Vaginosis Bacteria n.k husababisha
mwanamke kutokwa na uchafu
unaoambatana na harufu mbaya.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi
ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi
huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa
sehemu za siri usipozingatiwa hususani
mwanamke anapokuwa kwenye siku zake
za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya
bacteria wanaosababisha harufu mbaya.

 
 Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa
na dalili kubwa ya kutokwa na
ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu)
kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa
unatoa harufu kali kama shombo ya samaki
au kitu kilichooza na huambatana na
maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.
Wakati mwingine uchafu
wenye rangi kama ya kijani
hutoka
-Kuwashwa na
kuchomachoma sehemu za siri,
mgonjwa asipopatiwa tiba
haraka husababisha vidonda
sehemu za siri.
- Mwanamke anapoona
anatokwa na ute
uliochanganyikana na damu
hata kama hayupo kwenye
siku zake, hii ni dalili nyingine
ya Vaginosis.
- Maumivu makali wakati wa
tendo pia ni dalili za ugonjwa
huu.

Matibabu
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya
vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na
daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha
juu ya magonjwa ya wanawake. Dawa za
kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za
kumeza (Pills) huweza kumaliza tatizo hili.

Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila
kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa
daktari au nesi.

Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi
ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza
vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke
kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za
kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye
maji machafu ili kusafisha wenyewe
huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za
kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi
asali na vingine vingi naomba niseme kuwa
njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini
madhara yake ni makubwa kama hivyo
kuanza kutoa harufu mbaya.

Comments

Popular posts from this blog