TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHUO KIKUU CHA DODOMA (ADMINISTRATIVE STAFF)

Chuo Kikuu cha Dodoma kinawatangazia waombaji wa kazi mbalimbali kuwa usahili wa kuandika utafanyika Jumamosi ya tarehe 8 Machi, 2014 na Jumapili ya tarehe 9 Machi, 2014. Usahili huu utafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika kumbi za mihadhara ya Skuli ya Sanaa na Lugha kama ifuatavyo:
Jumamosi tarehe 8 Machi 2014
1. Maafisa Rasilimali Watu na Tawala
2. Maafisa Mipango 
3. Madereva 
4. Wahudumu 
5. Makatibu Muhtasi 
6. Wahudumu wa Afya

Jumapili tarehe 9 Machi 2014
1.Wahasibu Wasaidizi 
2.Wakaguzi wa Ndani Wasaidizi 
3.Watunza Kumbumbu Wasaidizi
4.Wasimamizi wa Mifumo ya Kompyuta Mtandao 
5.Wasimamizi wa Maabara

Usahili wa mahojiano kwa waombaji wa kada zote za afya isipokuwa wahudumu wa afya  utafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 10 Machi, 2014. Usahili huu utafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika jengo la Utawala kwa utaratibu ufuatao:-

Jumatatu tarehe 10 Machi 2014
1. Mafundi Wasaidizi wa Maabara 
2. Mafundi  Sanifu Maabara
3. Wasaidizi Kumbukumbu za Afya
4. Wahandisi Vifaa Tiba
5. Mafundi  Sanifu - Dawa
6. Mafundi Afya

Jumanne tarehe 11 Machi 2014
1. Wauguzi/Wakunga
2. Maafisa Uuguzi

Jumatano tarehe 12 Machi 2014
Madaktari

Alhamisi tarehe 13 Machi 2014
1.Wauguzi Wahitimu
2.Madaktari Bingwa

Usahili wa mahojiano kwa waombaji wa kada zote ambazo hazikuorodheshwa hapo juu utafanyika  Jumatatu na Jumanne yaani  tarehe 17  na 18 Machi, 2014 kama ifuatavyo:

Jumatatu tarehe 17 Machi, 2014
1. Wakufunzi wa Michezo 
2. Maafisa Sheria 
3. Waalimu Wakufunzi 
4. Maafisa Ugavi 
5. Mafundi  Mchundo
6. Wapokezi Wageni 
7. Wahandisi Maabara

Jumanne tarehe 18 Machi, 2014
1.Mafundi Sanifu 
2.Maafisa Miliki

ANGALIZO:
Siku ya usahili wasailiwa watatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti na vyeti halisi, vitambulisho au kadi za kupigia kura na picha moja ya pasipoti.
Tarehe za usaili kwa wanataaluma zitatangazwa baadae.

Comments

Popular posts from this blog