CCM YASHINDA KWA KISHINDO KIKUU JIMBO LA KALENGA

ush1Mbunge mteule wa  jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juu na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo  CCM imeshinda kwa  mbali katika matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye  jimbo la Kalenga  mkoni Iringa, Tume  ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Godfrey Mgimwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ambapo CCM  imeshinda kwa kura 22962  huku CHADEMA ikipata 5853 na chama cha CHAUSTA kura 150 Chama cha Mapinduzi  kimefanikiwa kushinda katika kata zote kumi na tatu za jimbo hilo.
Watu wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura na hali ilikuwa ni ya utulivu kabisa na watu wengi waliopiga kura wameishukuru serikali na tume ya uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na kufanyika kwa uchaguzi wenye utulivu..(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAlENGA)ush3Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akipiga picha na wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo wana CCM walifurika kushangilia ushindi  huo mnono ambao  CCM imeshinda kwa kishindo.
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
IMG-20140317-WA0001

Comments

Popular posts from this blog