BREAKING NEWS:BUNGE MAALUM LA KATIBA LAAHIRISHWA KUTOKANA NA VURUGU

 
Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Amelazimika Kuhairisha Bunge Jioni Hiii mara baada ya Kutokea Vurugu.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katika Jaji Joseph Sinde Warioba Alitakiwa kuwasilisha Rasimu ya Pili katika Bunge Hilo.Wajumbe wa Bunge Walipoingia Ukumbini Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Alipomwita Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mh Jaji Warioba ,

Wakati Mwenyekiti Huyo aliposimama Kuanza Kuwasilisha Baadhi ya Wajumbe waliendelea Kugonga Meza  kwa Nguvu Kuhu Wakizomea na Kusababisha Vurugu Ndani ya Ukumbi wa Bunge na Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Mh Samweli Sita alipojaribu Kuingilia Kati Lakini ILishindikana Na Ikalzaimu Kuliahirisha Bunge Maalum La Katiba Mpaka hapo
Atakapotangaza tena.
Mtafaruku huo ni baada ya Wajumbe na Baadhi ya wabunge wa upinzani kupinga Jaji warioba asiwasilishe rasimu ya katiba leo mpaka Rais ahutubie Bunge hilo kwanza.Mwenyekiti wa Bunge akaruhusu Jaji Warioba aendeleee na Uwasilishaji lakini wabunge wakaanza kujibizana na kupiga makofi na meza za bunge.Baadhi ya wajumbe wametoka nje na wengine wamebaki ndani huku wakiwa wamesimamaEndelea Kuwa nasi Kwa taarifa zaidi

Comments

Popular posts from this blog