AKAMATWA NA MENO YA TEMBO 2 YENYE UZITO WA KILO 15 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 22


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akionenyesha mbele ya waandishi wa habari Ofisi kwake meno ya tembo vipande 2 yenye thamani ya shilingi 22 hapo jana aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Batromeo Mtongwa hapo machi 8 katika kijiji cha kilida katika tarafa ya mamba wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na gobole 1 na risasi 14.SEK
 Mkazi wa kijiji cha mirumba kata ya kibaoni wilaya ya Mlele SAI LUPONJE (63) akiwa katika kituo cha Polisi mkoa wa katavi akielezea jinsi watoto wake wawili walivyomuua kitungulu Luhende (65) na kwisha kumtupa porini baada ya watoto wake wawili kukasirishwa na kitendo cha mama yao huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kitungulu Luhende ambae alikua ni hawara yake wa muda mrefu mauaji hayo yalitokea wiki iliyopita katika kijiji cha Milumba.
SEK
mkazi wa kijiji cha kilida tarafa ya mamba wilaya ya mlele Patromeo Mtongwa (58) akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi  baada ya kukamatwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14 mtuhumiwa alikamatwa hapo machi 7 mwaka huu majira ya saa mbili usiku nyumbani kwake katika kijiji cha kilida.

Na Walter Mguluchuma Mpanda  Katavi
Mtu mmoja  aliyefahamika  kwa jina la  Bathromeo  James  Mtongwa  58Mkazi wa Kijiji  cha Kilinda Tarafa  ya Mamba  Wilaya  ya Mlele Mkoa wa Katavi  amekamatwa akiwa nameno vipande viwili  vyenye uzito wa kilo 15  vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja na Bunduki moja aina ya Gobore na Risasi 14
Kwa  mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi  wa Mkoa wa Katavi Kamishina  mwandamizi msaidizi  mtuhumiwa  huyo alikamatwa  hapo  machi  7 mwaka huu majira ya saa mbili  na nusu usiku
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufutia taarifa ambazo ambazo zililifikia jeshi la polisi  pamoja na askari  wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kupata taarifa   kuwa mtuhumiwa  anamiliki nyara za Serikali  kinyume  cha sheria  ambapo  taarifa hizo zilipatikana   hapo  machi 6 kutoka kwa Raia wema
Alifafanua ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya  Katavi  walifika  kwenye kijiji  hicho cha Kilinda  nyumbani kwa mtuhumiwa  Batromeo  na kufanya  upekuzi  nyumbani kwa mtuhumiwa  na kufanikiwa  kukamata risasi 14
Kidavashari alieleza  wakati askari hao wakiendelea na upekuzi kwa kushirikiana na  uongozi wa kijiji    walilitilia shaka eneo moja  la nyumba hiyo  ya mtuhumiwa  kutokana na  eneo hilo kuonekana  kuwa limechimbwa
Alisema ndipo askari walipoamua kuchimba eneo hilo  na baada ya kufukua kwa kitambo kidogo  walifanikiwa  kukuta meno ya Tembo vipande viwili vyenye uzito wa kili 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 yakiwa yamefukiwa ardhini  kwenye shimo
Baada ya kukamatwa kwa  maneno hayo ya Tembo  polisi walianza kumhoji mshitakiwa  kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa akiifadhi  Silaha ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya  ujangili
Kidavashari  alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa  aliweza kueleza kuwa bunduki ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameifisha  kwenye eneo  linaloitwa King’anda lililopo  ndani ya Hifadhi ya Taifa  ya Katavi
Alisema siku ya   tarehe 8 machi   majira ya saa  nane  mchana  mtuhumiwa  aliwaongoza  Askari Polisi  na Askari wa Hifadhi ya Taifa  ya Katavi  na kuwapeleka  katika eneo la King’anda  ndani ya Hifadhi ya Katavi  na  aliweza kuwaonyesha silaha hiyo Bunduki  aina ya Gobore ikiwa imeifadhiwa  kwenye kichaka
Mtuhumiwa  anatarajiwa  kufikishwa  Mahakamani  wakati wawote  mara baada ya  upelelezi wa tukio hili utakapo kuwa umekamilika  mapema iwezekanavyo  pia jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  lanatowa wito kwa wananchi  kuendelea  kutoa  ushirikiano kwa jeshi la polisi  kwa kutowa taarifa za watu wanaojihusisha  na uwindaji haramu  wa rasilimali za Taifa ili kulinda  na kuhifadhi   rasilimali  zetu  kwa manufaa ya vizazi  vijavyo

Na Katavi yetu Blog

Comments

Popular posts from this blog