WATU WATANO MATATANI IRINGA WAKIWEMO WAWILI KUKAMATWA WAKISAFIRISHA MENO YA TEMBO


 

NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM,IRINGA
WATU watano wanashikiliwa na polisi mkoani Iringa kwa makosa mawili tofauti likiwemo la wakazi watatu wa dare s salaam kukutwa na pembe tano za ndovu maeneo ya kijiji cha ngenza kata ya ikweha tarafa ya sadani wilaya ya mufindi..
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kamanda wa polisi mkoa wa Iringa RAMADHANI MUNGI alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea januari 11.
Hata ivyo aliwataja watu hao ni RAJABU MARI (35), KADILI MOHAMED (27) na SALOME ALOYCE(50) ambao walikuwa wakitumia gari aina ya premio lenye namba za usajili T580 mali ya FROLIAN ELIUS mkazi wa Dar es S alaam walikutwa na pembe hizo zenye uzito wa kilogramu 37 ambazo thamani yake bado haijafahamika.
Wakati huohuo jeshi la polisi Iringa linawashikilia watu wawili majina RIZIKI KAFULILO (24) na MIRAJI NZOWA (28) wote wakazi wa mashine tatu manispaa ya Iringa kwa kosa la kukutwa na kete 16 za madawa.
MUNGI alisema tukio hilo lilitokea mnano tarehe 12 januari mwaka huu maeneo ya kirabu cha pombe za kienyeji ubena kata ya mivinjeni ambapo kete hizo zinazaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Aidha kamanda MUNGI alithibitisha kutokea kwa tukio jingine la mkazi wa luhunga tarafa ya ifwagi wilaya ya mufindi Jina JUSTINE LUWUNGO (22) ambaye ni mkulima kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kuiba kuku.

Comments

Popular posts from this blog