UBALOZI WAMTAPIKA JACKIE CLIEFF

HABARI mpya zinadai kuwa ubalozi wa Tanzania nchini China umegeuka ghafla na ‘kumtapika’ mwanamitindo Jacqueline Cliff Fitzpatrick aliyekamatwa nchini humo akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin kilo 1.1 Desemba 19, mwaka jana, tofauti na awali.

Mwanamitindo Jacqueline Cliff Fitzpatrick.
Kwa mujibu wa rafiki wa Jack ambaye huwa anampokea nchini humo aliyejitambulisha kwa jina moja la Chifu, mwanamitindo huyo alipokamatwa huko Macau, Hong Kong nchini humo, aliwasiliana na ubalozi huo ambao ulikiri kukamatwa kwa ‘video queen’ huyo wa video ya Nataka Kulewa.
“Nimeshangaa kusikia eti ubalozi hauna taarifa kuwa Jack alikamatwa. Mimi ndiye nilipiga simu ubalozini na kuuliza juu ya taarifa hizo ambapo walikiri kuwa na taarifa.

Jack baada ya kunaswa na dawa za kulevya nchini China.
“Labda waseme hawajapelekewa taarifa rasmi na Serikali ya China lakini ubalozi wetu Hong Kong unajua kila kitu,” alisema Chifu.
Akizungumza na redio moja Bongo, mtu aliyejitambulisha kuwa ni balozi wa Tanzania nchini humo alisema: “Uongozi wa hapa haujatujulisha chochote wala kutuandikia, kwa taratibu zetu sisi kama balozi, watu wote wanaokamatwa hapa kwa makosa ya aina yoyote ile serikali husika zinatuandikia, zikituandikia zinasema alikamatwaje na walichukua au watachukua hatua zipi.
“Kama wameshamfungulia mashitaka wanatujulisha, mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kutoka serikalini juu ya huyo Jack.”
Kufuatia taarifa hizo kumekuwa na utata wa kukinzana kwa kauli za ubalozini kati ya ile ya awali na sasa kuwa hawajui chochote huku ndugu wakikiri staa huyo kukamatwa China kwa kashfa ya unga.
Juhudi za Ijumaa Wikienda kuzungumza na balozi wa Tanzania nchini China, Abraham Shimbo ziligonga mwamba baada ya simu ya ofisini kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
GPL

Comments

Popular posts from this blog