Jaji aagiza Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Toroitich arap Moi afike kizimbani

 

Jaji Isaac Lenaola aliamuru ushahidi katika kesi utatolewa na wale walioshtakiwa binafsi mbele yake.

Hii inaamanisha kwamba Bw Moi atafika kortini kujitetea mwenyewe katika kesi hiyo aliyoshtakiwa na Bi Zipporah Seroney.
Hii ndiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Moi kufika mahakamani tangu ang’atuke uongozini. Atahojiwa na wakili anayemwakilisha mjane huyo: “Hii mahakama inaamuru kwamba kesi ya Bi Seroney itasikizwa mnamo Machi 25 na wakili wake ameagizwa ataoe samanzi kwa washtakiwa kufika kortini,”akaamuru Jaji Lenaola.
Bi Seroney na watoto wake watano wameishtaki Serikali na Bw Moi wakisema kama sio vitendo vya rais huyo mstaafu, mumewe aliyekuwa mbunge kati ya 1961 na 1975 hangekufa Desemba 1982.

Kulingana na wakili Gitobu Imanyara, marehemu Seroney alitiwa kizuizini kati ya 1975 na 1978 wakati Bw Moi alipokuwa makamu wa rais na baadaye alipotwaa hatamu za uongozi kutoka kwa hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Mjane huyo anadai kwamba mwanasiasa huyo aliendelea kuonewa na kudhulumiwa chini ya utawala wa Bw Moi hadi alipoaga.
Kubakwa
Bi Seroney anasema kwamba walifurushwa kutoka kwa nyumba yao na alipojaribu kurudi jitihada zake zilipingwa vikali 1991 kisha bintiye Christine Chepkorir akabakwa na genge la wanaume.
Mlalamishi huyo anasema bintiye aliumia na anaishi na fedheha.
Ameongeza kusema kwamba familia yake ilipoteza mali mengi kutokana na vitendo vya Bw Moi na maafisa wa utawala wa mkoa, maafisa wa usalama na maafisa wa upelelezi.
Bi Seroney alitorokea Amerika.
Bw Imanyara anasema katika kesi hiyo kwamba Bw Moi alitumia vibaya mamlaka yake kwa kuamuru Bw Seroney atiwe nguvuni na kuzuiliwa kwa muda mrefu

Comments

Popular posts from this blog