HUU NI MKASA WA KUSISIMUA WA KAHABA ALIYEOLEWA NA MCHUNGAJI NA KUPATA MIUJIZA:


MUST READ... BASED ON TRUE STORY<<<<<

Dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahida, alikuwa anafanya biashara ya kujiuza ili aweze kuweka kitu umboni mwake. dada huyo alikuwa na wateja wamaana na mapedeshee wengi sana kwa hiyo kwa siku yeye kuondoka na laki 4 au 5 kwa siku ilikuwa ni kawaida sana. siku moja dada Mahida
aliamua aende hospitali ili akatoe miamba aliyokuwa nayo tumboni mwake, alifanikiwa na kutoa mimba ile lakini baada ya kumaliza utoaji wa miamba alimuomba daktari atoe kizazi kabisa ili asipata tabu ya kuja kutoa mimba kila mara, daktari alifanya kama alivyoambiwa.
Dada Mahida alirudi mtaani na kuendelea na biashara ya kujiuza.

Siku moja ilikuwa jumapili Mahida alikutana na rafiki yake wa muda mrefu waliyekuwa wanaishi wote enzi za utoto wao, rafiki yake huyo alimwambia Mahida waende kanisani, ili kuficha aibu ya biashara aliyokuwa anafanya dada Mahida alikubari na wakaamua kwenda wote kanisani. Siku hiyo Mahida alielewa sana neno na akaahidi kuwa jumapili ijayo ataenda, basi ikawa tabia mpya ya dada Mahida akawa kila siku anafanya biashara zake za kujiuza na jumapili anaenda kanisani, kadri siku zinavyozidi kwenda dada Mahida akaanza kupunguza biashara ya kujiuza na kumgeukia Muumba mpaka akaacha kabisa tabia ya kujiuza na kuanza kufanya shughuli nyingine zilizokuwa zinamuingizia kipato.

Siku moja Mahida alienda kanisani na alipokuwa ameketi mchungaji alimfuata na kumwambia "nimeoteshwa kuwa ww ndiyo utakuwa mke wangu wa kufa na kuzikana" dada Mahida alishtuka na alimtazama mchungaji na kumwambia "mchungaji umekurupuka mimi kamwe siwezi kuwa mke wa mtu na kamwe siwezi kuzaa" alimaliza Mahida na kuondoka kanisani, kila wiki aliyokuwa anaenda kanisani dada Mahida alikutana na maneno yale yale kwa mchungaji na mchungaji alimwambia "nimeota umepata ujauzito na umenizalia watoto wanne" Mahida alimuangalia mchungaji na kusimama na msimamo wake ulele ule.

Siku zilizidi kuyoyoma lakini kutokana na mchungaji kuendelea kusema maneno yale yale basi ilibidi dada Mahida akubali na akakubali kuolewa na mchungaji na wakafunga ndoa na ndoa yao ilikuwa ya furaha sana. kadri siku zilivyozidi kwenda dada mahida alianza kuona mabadiliko mwilini mwaka na kuamua kwenda katika ile hospitali aliyowahi kwenda mwanzo kutoa mimba na kumkuta daktari aliyemfanyanyia utoaji wa mimba siku za nyuma, baada ya daktari kumona Mahida akajua amkekuja kwa shida nyingine ikabidi amuulize "Dada Mahida nikusaidie nini tena dada yangu" mahida alijibu kuwa anahisi anadalili za ujauzito, Daktari alicheka sana baada ya kuambiwa hayo majibu kutoka kwa mahida na daktari alimwambia "Dada mahida nona umechanganyikiwa enh dada yangu?? mimi ndiye nilitoa kizazi chako leo iweje uwe na mimba acha kuchekesha walionuna"

Mahida alimwambia daktari chukua vipimo kapime, kweli daktari alifanya hivyo na baadae akarudi mikono inamtetemeka na kumwambia mahida "Dada Mahida nipeleke na mimi kwa huyo uneyebuabudu nami niweze kumuabudu maana ni mkweli na anasaidia wanyonge, Dada Mahida ww ni mjamzito wa miezi miwili". Mahida alilia huku akiamini kuwa Mungu ashindwi na kitu chochote Duniani.
Daktari wiki ilifata naye alienda kanisani na kuanza kumtukuza muumba.

Ndugu yangu hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani lakini kumbuka yupo anaweza kufanya ugumu wa mambo yako kuwa mepesi kama unatafuna karanga.
hakunna kinachoshindikana kwa Mungu,

comment AMINA kama unaamini hakuna kinachoshindikana kwa jina lake yeye muumba na kama unaamini magumu yako yote yenaweza kuwa mepesi kupindukia.
Share na mwenzako kufikisha ujumbe

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK

Comments

Popular posts from this blog