CHUCHU HANS AIBIKA LIVE, WAMASAI WAHUSISHWA

STAA wa sinema za Kibongo, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufundishwa mila za kimasai na kusema ameelewa, muda mchache baadaye akachemka.


Chuchu Hans (kushoto)katika pozi.

Tukio hilo lililogeuka kituko, lilitokea hivi karibuni ambapo Chuchu akiwa na wasanii wenzake walifika katika Kijiji cha Misherani kilichopo mkoani Arusha kwenda kurekodi sinema lakini alivutiwa na mavazi ya kimasai ndipo alipoomba kujifunza mila za kabila hilo.

Akizungumza paparazi wetu, Chuchu alisema alipewa mtoto mdogo amfundishe namna ya kuvaa mavazi hayo ya Kimasai, akadai ameweza lakini alipopewa mara ya pili avae mwenyewe, alichemka.
“Daah! Niliabika maana mbaya zaidi nilielekezwa na binti mdogo nikamwambia tayari nimeweza lakini nilipokwenda kuvaa, nikavaa ndivyo sivyo, acha nichekwe,” alisema Chuchu.


Chuchu Hans (wa poli kutoka kulia) na watoto wa Kimasai.

Hata hivyo, baada ya kukosea huko, Chuchu alisema alijifunza upya na kuhakikisha kuwa ameweza hivyo kufuta aibu ya awali huku akiwasisitiza wasanii wenzake kujifunza mila tofautitofauti.

“Kujivunza mila tofauti ni jambo zuri katika maisha yetu hususan sisi wasanii, tunatakiwa kujua milia na tamaduni za kabila mbalimbali ili kuyawakilisha katika sinema zetu,” alisema Chuchu.


CDT:GPL

Comments

Popular posts from this blog