Posts

CCM YAPINGA UWEPO WA SERIKALI TATU....

Image
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita. Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili. “Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.   Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na

HATIMAYE THE PLATINUM AULA TENA

Image
Wanasema hela huenda kwa wenye hela na mwenye nacho huongezewa zaidi. Sina uhakika, lakini kwa mujibu wa picha nilizoziona kwenye akaunti ya Instagram ya Diamond Platnumz, inaonekana kama the lad is about get some serious money from wazee wa machapati ‘Azam’. Katika akaunti hiyo, Diamond ameweka picha kadhaa ambazo zote zinamuonesha akiwa amebeba magunia ya unga wa ngano wa Azam na katika picha moja ameandika, “Guess what???. Tutegemee surprise siku si nyingi!!

HUU NDO MJENGO UNAOSEMEKANA KUWA NI WA MCHUNGAJI MTARAJIWA a.k.a MASANJA

Image
MJENGO WA MSANII MASANJA ULIOPO JIJINI DSM

FAMILIA YA NGWEA YAMKATAA MTOTO WAKE ALIYELETWA NA MAMA YAKE MAKABURINI

Image
Siku chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao yanazidi kuibuka.  Mtoto wa Ngwea akiwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa mazishi ya baba yake. Habari zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea. Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo. Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo. Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumw

YULE MUUAJI WA DADA ALIYECHINJWA KAMA KUKU UKO MIKOCHENI "B" HATIMAYE APATIKANA

Image
MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30).  Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita.  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B. “Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’, katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). “Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova. Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijuma

WAKENYA WALIVYOANDAMANA JUNE 11 NA KINYAGO CHA NGURUWE NA DAMU WAKIPINGA MISHAHARA YA WABUNGE

Image
Miungano ya kijamii ikiongozwa na Bunge la mwananchi,Muhuri na pawa 254 miongoni mwa mengine yameandaa maandamano ya pili kupinga juhudi za wabunge kuhujumu tume ya kuratibu mishahara nchini kenya SRC ili kujiongezea mishahara ya hadi laki nane kinyume na ilivyopendekezwa na SRC. Tofauti na wiki kadhaa zilizo pita ambapo waandamanaji waliwaelekeza nguruwe walioandikwa majina ya wabunge walio unga mkono mswada huo, hii leo waandamanaji walibeba kinyago wa nguruwe na damu walio ashiria mwisho wawabunge kukandamiza wakenya. huku wakijimwagilia damu kama ishara ya kuumizwa na kodi ya kuwalipa wabunge.  Waandamanaji pia walibeba mfano wa noti za shillingi alfu moja pesa za kenya zilizo chorwa Nguruwe mkubwa kwa upande mmoja na wanawe kwa upande wa pili, huku wakiwarushia wabunge noti hizo kuashiria kujitakia makuu kwa wabunge hao. Viongozi wa waandamanaji wameahidi kuendeleza maandamano hadi pale wabunge watakapo sitisha hujuma dhidi ya tume ya bi sar

MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE ( KASHI ) ALIYEFARIKI JANA

Image
              Pichani juu ni mazishi ya msanii ya mwigizaji  Jaji Khamis 'Kashi' aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar yaliyofanyika leo mchana majira ya saa nane kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Marehemu Kashi alikumbwa na umauti baada ya kuugua ghafla malaria na kifua. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Kashi mahali pema peponi. AMEN!

: NIKIFA ASHA BARAKA ASIJE KWENYE MAZISHI YANGU- ALLY CHOKI

Image
Huu ni ugomvi mwingine mpya wa wasanii wetu na haya ni maneno aliyosema mkurugenzi wa Extra Bongo ALLY CHOKI ATOA KAULI NZITO: “NIKIFA ASHA BARAKA ASIJE KWENYE MAZISHI YANGU” … “Katika watu nisiowapenda kabisa ni Asha na Baraka Msilwa”  ASHA BARAKA NAYE AJIBU MAPIGO: “HAYO NI MAMBO YA KIKE” …“Wamanyema peke yake wanatosha kunizika, amtaka Chocky akapime kwanza MKURUGENZI wa Extra Bongo Ally Chocky ametoa kauli nzito kuhusu waajiri wake wa zamani, Asha Baraka na Baraka Msilwa. Katika maongezi yake mahususi na Saluti5 Chocky alisema katika watu asiowapenda duniani ni Asha Baraka (Mkurugenzi wa ASET) na Baraka Msilwa (Mwenyekiti wa ASET). Asha Baraka na Baraka Msilwa ni mtu na kaka yake. TOA MAONI YAKO

KWELI UALIMU KAZI -"MWANAFUNZI MMOJA WA KIKE AMTAKA MWALIMU WAKE KIMAPENZI"

Image
Mimi  ni mwalimu wa shule moja  ambayo sitaitaja. mwezi uliopita mwanafunzi wangu wa kike ambaye  yuko  kidato  cha  tatu alinifuata na kuniambia anataka kunipa zawadi... Sikuwa na hili wala lile, hivyo nilimwambia ni poa tu kama ameamua  kunikumbuka mwalimu wake.. Zawadi aloniletea ilinifanya  nishike  kichwa maana  sikutegemea.Yule mwanafunzi  aliniletea chupi aina ya boxer 3  na  tangu siku hiyo kila akiniona ananifanyia vituko mpaka ananikalia nusu  uchi  darasana nikiwa nafundisha  kwa vile anakaa viti vya Mbele.... Nikiwa  kama  mwalimu, nimejaribu  kutumia  viboko  ili  kumuonesha  kwamba  sina  mpango  naye lakini  bado  imeshindikana.. Nifanyaje  ndugu  zangu?  Maadili  ya  kazi  yananibana.Hata  hivyo, mwanao  ni  mwanetu  sote.

MSANII H. BABA NA FLORA MVUNGI HATIMAYE WAFUNGA NDOA....

Image
. BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi, wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu. H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.   Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo. “Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora. Flora akimnywesha mumewe kinywaji. Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha. H Baba akisaini kitabu cha ndoa. Akizungumza na mwandishi  wetu, H. Baba alifunguka kuwa ali

CHAMA CHA DEMOKRASIA(CHADEMA) WAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA MPYA

Image
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na Jaji Joseph Warioba. Mwenyekiti huyo alikuwa akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji la Mbeya katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Iyela kwa tiketi ya Chadema Charles Nkelwa. Kiongozi huyo wa upinzani bungeni amesema sababu kubwa ya kuunga mkono rasimu hiyo ni kwamba mambo mengi yaliyoorodheshwa na chama hicho yamekubaliwa. Mbowe amesema jambo kubwa lililofanyiwa kazi ni kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika. Mbowe amesema amesikitika kuona baadhi ya wanaCCM wakiipinga serikali ya Tanganyika na kung'ang'ania serikali mbili na kudai watu hao ni wanafiki wanaopaswa kupuuzwa na wananchi. Kauli ya Mbowe imekuja wakati ambapo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dr Kitila Mkumbo alinukuliwa kusema rasimu mpya ya Katiba iliyotolewa na Warioba ni bora mara mia mbili akilinganisha na katiba ya sasa. Mara baada ya mkutano huo maelf

KADI ZA CCM ZARUDISHWA HUKO MOROGORO....TUNDU LISSU AZICHOMA MOTO HADHARANI

Image
Baada ya kutoa hotuba nzito na zenye kugusa matatizo ya wananchi, wananchi hao walirudisha kadi zao na kwa kuwa kadi hizo lissu hakuja nazo akazichoma moto.

CIARA ASHTAKIWA NA BAR YA WATU WENYE KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA

Image
Mwanamziki Ciara  ameshtakiwa na bar inayohudhuriwa na watu wanyekushiriki mapenzi ya jinsia moja (gay), iliyoko West Hollywood, ambao wanadai kuwa mwanamziki huyo aliwaacha kwenye mataa pale alipojitoa katika moja ya tamasha lao walilotarajia kulifanya leo usiku (7th)   Club hiyo ya usiku inayoitwa " The Factory " inasemekana kuwa inajaza sana wateja wake hao ambao wanajua ku-party  kutokana na mshtaka hayo, Ciara ali-sign dili la dola za kimarekani 10,000 kutokea katika bar hiyo leo usiku, ikiwa ni siku moja kabla ya kufanya show kwenye L.A. Pride parade.  Factory wanasema kuwa Ciara amesema kuwa hataweza ku-perfome kutokana na kizuizi kilichopo kwenye mkataba wake aliosaini na tamasha la  Pride na kuendelea kusema kuwa bila kutarajia mwanadada huyo alijitoa siku ya tarehe 3 june, na kuwaacha wakiwa hawana star yoyote kwenye bash hiyo kabla ya pre gay parade bash Kwasasa bar hiyo inamshtaki Ciara kwa kukatisha mkataba na kumtaka alipe h

STULI/KIGODA CHA MWENGE WA UHURU CHAIBIWA JIJINI ARUSHA....

MTAZAME SNURA AKIFANYA MAMBO YAKE KWENYE STAGE FULL KUJIACHIA

Image
 Naamini kwapicha hizi uwezi kosa show yake jumapili hii NEW MAISHA CLUB atazindua video yake ya majanga kuwa mjanja kuwa wa kwanza kuiona, atasindikizwa na WEMA SEPETU atakata utepe wa video ya majanga,MIRROR,SAMIR,ALI NIPISHE,TIMBULO,BAUCHA,MENINAH, na MADEE kiingilio 10,000 tu hii show sio yakukosa kabisa.

TAZAMA PICHA 9 ZA UNYAMA WA SNURA KWENYE STAGE, NI MAJANGA KWELIKWELI

Image
 Naamini kwapicha hizi uwezi kosa show yake jumapili hii NEW MAISHA CLUB atazindua video yake ya majanga kuwa mjanja kuwa wa kwanza kuiona, atasindikizwa na WEMA SEPETU atakata utepe wa video ya majanga,MIRROR,SAMIR,ALI NIPISHE,TIMBULO,BAUCHA,MENINAH, na MADEE kiingilio 10,000 tu hii show sio yakukosa kabisa.

RAIS KIKWETE AMFARIJI MALKIA WA MIPASHO ( KHADIJA KOPA ) KWA KUFIWA NA MUMEWE

Image
  Rais Dk. Jakaya Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Kopa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita. Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwafariji wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM,  Hadija Kopa kufuatia kifo cha mumewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Ahmed Kipozi na (kulia) ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa CCM, Ridhwani Kikwete.