TAMBO MPYA ZA NEY WA MITEGO

Stori: Musa
STAA wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, hivi karibuni alifunguka kuwa hakuna jambo analoepukana nalo kama kukutwa na mchumba wake, Siwema akiwa na mademu wengine maana huwa anazimia.

Akipiga stori na paparazi wetu Desemba 13, mwaka huu, Nay alisema kwamba pamoja na usanii wake wote na kuwa karibu na mashabiki wa muziki wake, amekuwa akijiepusha sana kwenye suala zima la kuwa karibu na mademu kwani hapendi kumsababishia Siwema matatizo ya kuzimia.
“Mchumba wangu ananipenda sana na ndiyo maana sasa ninaishi kwa tahadhari kubwa kwani sipendi kumuona Siwema wangu akizimia kwa sababu ya wivu, najitahidi kumlinda kwa kujiepusha kuwa karibu na mademu,” alisema Nay.

Comments

Popular posts from this blog