SHIJA AMPIGA DONGO WASTARA

STAA wa filamu Bongo, Deogratius Shija amesema katika maisha yake hafikirii kutoka kimapenzi na mwanamke yoyote ambaye ni msanii hususani kuingia naye katika maisha ya ndoa.
Deogratius Shija.
Akizungumza na paparazi wetu alisema, kamwe hawezi kukurupuka akajiingiza mkenge kumuoa msanii kwa kuwa hana imani na wasanii wa kike na hajawahi kujihusisha nao kimapenzi, kwani  mastaa wengi ni walaghai wanaumiza vichwa.
 
“Nawaza sana mwanamke wa kumuoa kwa sasa lakini suala la kuoa msanii halipo kabisa, nashangaa hata wale wanaonishauri nimuoe Wastara siwezi kukurupuka kiivyo simjui undani wake kikubwa ni kumuomba Mungu anipatie mke mwema,”alisema Shija.

Comments

Popular posts from this blog