RAIS JAKAYA KIKWETE ALIHUTUBUA TAIFA KUPITIA BUNGE MJINI DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akilihutubia Bunge mjini Dodoma leo.
Rais Jakaya Kikwete akiendelea kulihutubia Bunge..
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,akiwasili katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo

Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge mjini Dodoma na kueleza kuwa Serikali ya Tanzania haiko tayari kujitoa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
 
Rais Kikwete alibainisha kwamba kumekuwa na vikao visivyo rasmi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Rwanda ambavyo vimekuwa vikipitisha mambo yao bila kushirikisha nchi nyingine ndani ya Jumuiya ambazo ni Tanzania na Burundi.
 
“Wenzetu wameshafanya vikao vitatu na kupitisha maamuzi manane ya kushirikiana, kwetu sisi tunadhani hizi ni fujo za kutaka kuhatarisha uhai wa maisha ya jumuiya yetu ya Afrika Mashariki," alisema Rais Kikwete.
 
Alisema Tanzania itaendelea kuheshimu mambo yaliyomo kwenye makubaliano ya uanzishwaji wa jumuiya hiyo ambayo ni umoja wa forodha, soko la pamoja, sarafu ya pamoja na shirikisho la kisiasa bila kukiuka mlolongo wa utekelezaji wake.
 
Mbali na suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia Rais Kikwete alizungumzia suala la wanajeshi waliokwenda nchini Congo DRC kulinda amani, Operesheni Tokomeza dhidi ya ujangili na mchakato wa Katiba Mpya

Comments

Popular posts from this blog