MWILI WA MAREHEMU DK.MVUNGI WAPOKELEWA KWA MAJONZI JIJINI DAR ES SALAAM NAKUTOLEWA RATIBA KAMILI YA MAZISHI

 Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
 Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi................
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
 Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe
Ndugu wakilia kwa uchungu...
Na Father Kidevu Blog
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.

Makumi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.

Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba 2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.

Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi.  Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.
________________
MUDA
TUKIO
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK
NYERERE
Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa
mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
Saa 2:00 – 3:30
asubuhi
Kuwasili kwa
Wageni, Wananchi na Waombolezaji
Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili
wa Marehemu
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa
Takatifu, Viwanja vya Karimjee
Saa 5:45 – 6:55
mchana
Salaam za
Rambirambi na Neno la Shukurani
Saa 6:55 – 8:40
Mchana
Kuaga Mwili wa
Marehemu
Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka
mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU
- KIBAMBA, MSAKUZI
Saa 2:30 – 4:30
asubuhi
Ibada ya Misa
nyumbani kwa marehemu
Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya
kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro

Comments

Popular posts from this blog