Mahakama yatoa hati ya kukamatwa kwa Wema Sepetu haraka


Mahakama ya mwanzo Kawe jijini dar es salaam imetoa hati ya kumkamata miss tanzania 2006 Wema Sepetu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni dharau ya wito wa mahakama hiyo. 
 
Chanzo cha ndani kilichoomba kuhifadhiwa ya jina kimempasha mwandishi wetu kuwa hati hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wema kushindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo na bila kutolewa udhuru wowote. 

Aidha imeelezwa kwamba mahakama hiyo pia imetilia mashaka udhuru uliotolewa septemba 30 kwamba wema ni mgonjwa baada ya kuvuja kwa picha katika mitandao zikimuonyesha Wema akila bata  Hong Kong China na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Diamond. 

Wema alitolewa udhuru huo na kijana aliefahamika kwa jina la Martini .
 Kesi inayomkabili wema katika mahakama hiyo ni ya kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumpiga meneja wa hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe beach jijini Dar es salaam bwana Godluck kayumbu. 

Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu alimtafuta mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Kayumbu na kumuuliza kuhusu hati iliyotolewa na mahakama ambapo alithibitisha kuwepo kwa jambo hilo. 

Bwana Kayumbu alisema kuwa amepewa hati  maalum ya kumkamata wema octoba 30 mwaka huu ambayo kesi hiyo ilitajwa tena mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu anaweza kukamatwa muda wowote kuanzia sasa kwani octoba 30 mwaka huu kesi hiyo ilitajwa tena mahakama ya Kawe chini ya mheshimiwa hakimu Ikanda lakini wema hakutokea na hakuna mtu yeyote aliyekuja kwaajili ya kumtolea udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa mshtakiwa wake wema sepetu hakuja mahakamani mara mbili mfululizo kuanzia septemba 30 2013 na kudaiwa kuwa anaumwa lakini picha zake katika mitandao zilimuonyesha  akitanua hong kong china na mara ya pili kesi hiyo ilitajwa octoba 30 2013 ambapo hakutokea mtu yeyote anayemuhusu wema katika mahakama hiyo. 

"Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa lakini nilikuwa peke yangu sasa nikaamuliwa mimi nipewe hati maalum ya kumkamata wema ambapo nilipewa na nimeshaikabidhi kituo cha polisi cha kawe kwa utekelezaji maana naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi," alisema kayumbu.
Mwandishi  wetu alipomtaarifu bwana kayumbu kuwa octoba 30 Wema Sepetu alikuwa kwenye msiba baada ya kufiwa na  baba yake mzazi mzee Isaac Sepetu na kwamba siku hiyo alikuwa safarini kwenda zanzibar kwa ajili ya mazishi ya mzazi wake huyo, bwana kayumbu alisemaa kuwa suala hilo halimuhusu kwani hata yeye amefiwa na wazazi wake. 
"Kama kafiwa hata mimi nimefiwa na baba na mama yangu pia, kinachotakiwa ni kutii sheria za nchi ikiwemo mahakama ,kama alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina mazungumzo tena kinachotakiwa ni sheria ichukue mkondo wake, popote atakapopatikana wema ni lazima akamatwe," alisema Godluck. 
Wema hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia jambo hilo.

Comments

Popular posts from this blog