KIMBUNGA 'HAIYAN' CHADAIWA KUUWA ZAIDI YA WATU 10,000 NCHINI PHILIPPINES, VIETNAM NA CHINA WAANZA KUJIPANGA

Kijana akiangalia maafa yaliyosababishwa na kimbunga jijini Tacloban nchini Philippines.
Nyumba pamoja na boti vikiwa vimeharibiwa…



Kijana akiangalia maafa yaliyosababishwa na kimbunga jijini Tacloban nchini Philippines.

Nyumba pamoja na boti vikiwa vimeharibiwa eneo la Iloilo nchini Philippines.


Jiji la Tacloban nchini Philippines baada ya kukumbwa na kimbunga 'Haiyan'.


Mama huyu akiwa katika jengo lililobomolewa na kimbunga.

Mtoto akijaribu kumpatia msaada mwenzake baada ya kimbunga hicho jijini Tacloban.

Gari likiwa limepinduka baada ya kimbunga jijini Tacloban.

Famili hii ikijaribu kujihifadhi wakati wa kimbunga eneo la vijijini nchini Philippines.

Wananchi wa Philippines wakisubiri misaada katika jiji la Sorsogon.

Wanajeshi nchini Vietnam wakiwashusha wananchi kutoka kwenye lori wakati wakiwahamishia katika maeneo salama kujikimga na kimbunga.

Wakazi wa Phu Yen, Vietnam, wakiandaa viroba vya mchanga kwa ajili ya kuweka juu ya paa za nyumba zao kujikinga na kimbunga.

Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Vietnam wakiweka mifuko ya mchanga juu ya paa za nyumba ikiwa ni tahadhari dhidi ya kimbunga.

Wavuvi wakiondoa boti zao katika fukwe nchini Vietnam ikiwa ni tahadhari ya kimbunga.

Maeneo yatakayokumbwa na kimbunga.

(PICHA ZOTE: EPA, AP NA REUTES)
-Red Cross wasema watu zaidi ya 1,200 wamepoteza maisha, 1,000 kati yao ni kutoka jiji la Tacloban, Leyte
-Watu milioni nne waathirika na kimbunga hicho
-Miili yatapakaa mitaani, waokoaji walinganisha maafa hayo na Tsunami ya mwaka 2004
-Kimbunga hicho kinaelekea nchi za Vietnam na China
-Mamilioni wayahama makazi yao
-China na Vietnam wajipanga kukabiliana na kimbunga hicho

VIFO vilivyotokana na kimbunga kikali 'Haiyan' kilichoikumba nchi ya Philippines juzi Ijumaa vinadaiwa kufikia 10,000 imeelezwa.
Mpaka sasa taarifa kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu zinasema watu 1,200 nchini Philippines wamepoteza maisha wakati wengi wakijeruhiwa lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka.
1,000 kati ya waliopoteza maisha wanatoka jiji la Tacloban na kisiwa cha Leyte wakati 200 wakitokea Samar.
Kimbunga hicho kinatarajia kuikumba nchi ya Vietnam leo na baadaye China kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa. Wananchi wa Vietnam na China wanachukua tahadhari kwa kujikinga na madhara yanayoweza kutokana na kimbunga hicho.

Comments

Popular posts from this blog