Dk.Sengodo Mvungi aliyevamiwa na kukatwa mapanga afariki dunia



Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
 
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini
TUNAPENDA TOA  POLE KWA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI. BWAna KATOA NA BWANA KATWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Comments

Popular posts from this blog