wanafunzi takriban 50 wanusurika katika ajali jijini dar es salaam jana jioni



Askari wa usalama barabarani wakijipanga kutoa huduma baada ya basi la daladala lililokuwa limebeba wanafunzi takriban 50 wa shule ya msingi ya Mgulani kugongana na gari dogo aina ya RAV 4 na kupinduka katika makutano ya Kenyatta Avenue na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam jana jioni.

Dereva wa gari dogo akiwa na mtoto wa umri wa takriban miaka mitatu walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali. Wanafunzi wote walinusurika.
Uharibifu wa miundumbinu baada ya ajali hiyo
Askari wa usalama barabarani wakiondoa mabegi ya wanafunzi hao ambao walitafutiwa basi lingine kuwapeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi
Wanafunzi wakiwa katika gari walilotafutiwa baada ya ajali hiyo
Magari ya break-down yakifanya juhudi ya kunyanyua basi hilo
Baadhi ya wanafunzi hao baada ya ajali. Ishukuriwe hakuna aliyeumia
 
KAMA UMEGUSWA TOA POLE KWA KUSEMA "AMEN" KISHA LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK

Comments

Popular posts from this blog