RUFAA YA BABU SEYA, PAPII KOCHA KILICHOBAKI NI HUKUMU TU BAADA YA KESI KUPITIWA UPYA

Leo, Jumatano, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania limeipitia upya hukumu yao.

Katika rufaa hiyo leo wakili wa Babu Seya na Papii Kocha ameiomba mahakama hiyo ifute ushahidi na waachiwe huru lakini serikali imepinga. Kutokana na hatua hiyo, leo mahakama ya rufaa haijafanya uamuzi wowote imewapiga kalenda na kesi inasubiri hukumu mpya.

Nguza Viking na Papii Kocha wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

Nyuso za matumaini.......
Johnson Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.
Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.

Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza wakati wakitoka mahakamani.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.
Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.
Mahakamani.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.

Comments

Popular posts from this blog