Mzee Majuto atangaza kujitosa kugombea ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM



Kwa mujibu wa mtandao wa Bongomovies, msanii mkongwe wa vichekesho hapa nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Tanga Mjini mwaka 2015


Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds na amedai kwamba atagombea kupitia CCM.

Juhudi za kumtafuta mzee Majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni za kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini zinafanyika...

Comments

Popular posts from this blog