Mlimani City yaanza KUWASACHI watu wanaoingia ndani baada ya taarifa kuzagaa kwamba lile GAIDI la kike liko Dar limejificha

phars

Katika hali tofauti waliyokutana nayo wanunuzi wa bidhaa kutoka kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye mall ya Mlimani city, wengi wameona ni hatua nzuri baada ya kuongeza usalama wa watu wanaotumia jengo hilo hasa kutokana na mambo yaliyotokea huko Kenya.

Tofauti na jana, leo hii jumapili 6/10, wateja wote waliokuwa wanaingia kwenye mall hiyo walikuwa wanasachiwa na mashine maalum pamoja na mabegi yao.

Mdau wetu alifika kwenye mall hiyo kwa manunuzi ya kawaida na alikuta askari wanaohusika na ulizi wakiwa wametengenisha njia mbili, moja ya kutoka na nyingine ya kuingia kwenye kila mlango wa kuigia kwenye mall. Askari wawili mmoja wa kike kwa ajili ya wateja wa kike na mwingine wa kiume pamoja na askari wa tatu kwa ajili ya kusachi mabegi.

Baadhi ya watu walionekana kufurahia hatua hiyo ambapo siku kadhaa zilizopita, watu wengi walianza kujiuliza maswali juu ya usalama wa watu wanaongia kwenye mall hiyo kwa ajili ya manunuzi yao ya kila siku.

Comments

Popular posts from this blog