"BREAKING NEWZ"MWANDISHI UFO SARO WA ITV AJERUHIWA KWA RISASI


download

Habari zilizotufikia zinasema Mwandishi wa habari wa ITV Ufo Saro ambaye anaonekana pichani kulia akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika moja ya kazi zake za kiuandishi amejeruhiwa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo hata hivyo bado taarifa rasmi za chanzo cha tukio hilo hakijafahamika, phars blogspot imeongea kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema bado hawajajua chanzo hivi sasa wanakimbizana kujua hali ya majeruhi na vipi atapa huduma za matibabu ambaye amalazwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi,
Tunaendelea kufuatilia na kujua taarifa kamili mara tutakapokuwa tayari tutawajulisha kupitia ukurasa huu.
TUTAENDELEA KUKUJUZA ZAIDI

Comments

Popular posts from this blog