YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA KATIBA JANGWANI

DSC_0429_eb0cb.png


Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo
DSC 0427 debe5

FREEMAN MBOWE.
KOSA kubwa kuliko yote katika kudai haki ni woga. katiba haitapatikana kama tunaendelea kuwa waoga na wenye hofu. makundi mengi nje ya bunge yana hekima na busara. tunahitaji kukutana nao ili kuunganisha nguvu kudai katiba.
way foward;
-kuunganisha makundi nje ya bunge
- sheria iliyopitishwa lazima irekebishwe.kama haitarekebishwa wapinzani watasusia mambo mengine yote.
-polisi wamezuia maandamano: hatutaendelea kuwa kondoo.maandamano ni haki kwa hiyo tarehe 10.10 kuna maandano makubwa kudai katiba. NCHI NZIMA. modus operandi itatangazwa.
-viongozi wa dini wasaidie kuhubiri umuhimu wa katiba
-ccm wanaoona umuhimu wa katiba wanakaribishwa.
-katiba inapaswa kutuunganisha. tarehe 10 oct itakuwa siku ya civil disobedience.
-jumatano ijayo mkutano zanzibar.
-sasa hakuna kuongea na kikwete.PICHA NA HUDUGU NG'AMILO
DSC 0401 7879d
DSC 0402 4ff40
DSC 0422 add19
Mbatia: Kitendo cha Zanzibar kufanya marekebisho makubwa ya Katiba ya Zanzibar kimeleta mgogoro mkubwa wa kikatiba maana maana Katiba hiyo imemnyang'anya kabisa rais wa muungano madaraka yake ndani ya JMT.
Anasema kuna shinikizo ndani ya CCM na serikali yake kuwa kama rais hata saini rasimu hiyo basi atasababisha kutokea kwa mgogoro mkubwa wa kikatiba hapa nchini, wakati tayari ndani ya nchi tuko kwenye mgogoro wa mkubwa kikatiba baada ya kitendo cha Zanzibar kufanya marekebisho hayo ya Katiba hiyo.
Mbatia anakumbusha kuwa si vema kwa bunge hili kuachiwa kututungia Katiba maana lenyewe ni mtoto wa Katiba; mtoto hawezi kumzaa mama, bali mama ndiye anayetakiwa kumzaa mtoto.
Anasema Katiba inatakiwa ipatikane kwa maridhiano yanayptakiwa yafikiwe na makundi yote ya kijamii; na maridhiano hayo hayapaswi kufanywa baada ya machafuko, bali yanatakiwa yafanyike sasa!
Askofu Kakobe: Mikutano hii isiitwe ya wapinzani maana watu kama yeye hawatakubali kuhudhuria maana yeye sio mpinzani bali mtanzania; hivyo viitwe vikao vya wananchi.
Kakobe kamtahadhalisha rais Kikwete kuwa huu ndio mtihani wake wa mwisho, kama atasaini mswaada huo, pamoja na kelele zote zinazopigwa na watu wote hao; basi atakuwa ameferi mtihani huu wa mwisho kwake!
Lipumba: Serikali ya muungano inaidharau serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Wamefikia mahali pa kumdhalilisha hata makamu wa pili wa rais wa Zanzibar kwa kumuita kwa simu ili aje athibishe kuwa walishirikishwa; kitendo cha yeye kukubari ulaghai huo kumemfanya aonekane kituko huko kwao Zanzibar maana alikubali vitu ambavyo hata hakusoma!
"Hawa maCCM ni balaa zaidi, maana wamemdhalilisha hata mwana CCM mwenzao!"
Mnyaa: Wabunge wa CCM waliopitisha marekebisho ya sheria ya katiba mpya hawakufikisha akidi ya kuweza kupitisha muswada huo; hivyo rais asiusaini maana sio halali!
Mnyaa: Zanzibar ni mshirika wa muungano huu, sio rafiki tu wa muungano kama inavyofiri CCM.
Kitendo cha kamati ya katiba kutokwenda Zanzibar ni kuikejeri Zanzibar; CUF pamoja na vyama washiriki wao na wadau wote hawako tayari kuivumilia kejeri hiyo!
Tundu Lissu
anaanza kusema kuna haja kuendelea na ugomvi wa dodoma.hatutakubali ccm kuchakachua katiba. hatukukubali dodoma wala hatutakubali popote kutungiwa katiba na ccm, wajumbe wa kamati wasiokuwa Maccm waliitwa wiki 2 kabla ya wengine.
kuwezesha kusikiliza maoni ya wadau nje ya serikali.wote kutoka Tanganyika. hakuna mzanzibari hata mmoja. kwa hiyo hakukuwa mzanzibar wala kiongozi yeyote.
muswada ukasema kikwete ateuwe wajumbe 166 wasiyo wabunge. kwa bunge la sasa maccm yana 72% ambayo tayari ni theluthi mbili tayari.halafu mwenyekiti wa maccm ateuwe tena maccm wenziye.tukakataa.
Muungano.
muungano ni kati ya washiriki sawa.wajumbe bunge maalumu linatoa asilimia 30 tu zanzibar.kwa nini washiriki sawa wawe siyo sawa kwenye bunge sawa?? na kwa nini tume ya katiba wajumbe waliku sawa kwa sawa??
Maccm yakakaa dodoma.yakaona tukiruhusu watu wote kutengeneza katiba maccm yataondolewa.kwa hiyo tutumie rais kuchakachua. kutumia bunge la katiba kuziba mdomo tume ya warioba. wapinzani tukatoka nje kupambana nje. tukiruhusu utaratibu huu tutapata katiba ya ki ccm ccm. hawataki mabadiliko yoyote ya msingi. tukiwaruhusu itakula kwetu
Mabere Marando!!! kwa niaba ya Dr.Slaa
1. watanzania leo wamevutwa na muungano wa ushindi wa upinzani
2.Dr.Slaa anasema kikwete amejipa jukumu kuunda katiba mpya. siyo bora katiba
3. bila katiba mpya kikwete ataacha nchi katika mgogoro.kwa hiyo atumie busara
kaimu katibu mkuu nccr anaongea. kutangeneza katiba siyo tukio ni mchakato unahitaji kuwa vumilivu.anasoma ibara ya 21 ya katiba ya sasa.
kutunga katiba siyo hisani ni haki ya watu. yeye anasema anaunga mkono rasimu hii kwa asilimia nyingi.
anaongea changamoto; watawala wanaweweseka mambo yanayoweza kutugawa.tujadili hayo .
1 muungano
2 udini
tuwe macho na mchakato
Mbunge wa mtambile cuf masoud salim toka pemba.kwa niaba ya wabunge wa cuf. wataendelea kutafuta katiba ndani na nje ya bunge.bila kujali itikadi cuf inawaunganisha wananchi wananchi kukataa uonevu.kitendo cha kamati ya sheria kutoenda zanzibar kwa wadau ni chukizo zanzibar watu wamekufa wakidai katiba na historia hiyo tunaendelea nayo
Mnyika anaongea kwa nia ya wabunge wa chadema. watawakilisha matakwa ya wananchi bungeni na hata  mtaani. wamekuwa wanasusia bunge ili kulazimisha katiba mpya. wamepeleka kanyaboya na sasa wameungana na mahakama ya watu kwani ndiyo mamlaka ya mwisho.
mbunge buyogera wa nccr kasulu. anajinasibu kama kamanda wa mageuzi.anawaomba wamama wasimame kuwasapoti viongozi kudai katiba itakayolinda wote hasa wamama na watoto. katiba ni mali ya wote na ndo inapanga maisha ya wanadamu kwa hiyo tusilete mchezo amepongeza kuacha kujali itikadi

Comments

Popular posts from this blog