Odama: Sijahongwa..vifaa vya kisasa kwa ajili ya utengenezaji filamu.

Miezi kadhaa ikiwa imepita tangu mtayarishaji na mwigizaji wa filamu nchini Jennifer Kyaka ‘Odama’ kuanza kumiliki vifaa vya kisasa kwa ajili ya utengenezaji filamu, amesema kitu kinachomuumiza zaidi ni kwa baadhi ya watayarishaji kuamini kwamba fedha wanazotumia waigizaji wa kike kuandalia filamu wamehongwa.
 
Akizungumza Odama alisema hata maendeleo yake hayajatokana na kuhongwa.

Anaongeza kuwa watayarishaji wa kike wamekuwa na changamoto nyingi sana katika uandaaji wa filamu nchini, lakini yeye ni mwanamke wa shoka kwani anajiamini kwa kile anachokifanya.

“Kinachoniumiza ni hawa wenzetu kuamini kuwa watayarishaji wa kike fedha zao za kupewa na hawana uchungu nazo, hata wakipatana na wasanii kucheza katika filamu zao gharama huwa kubwa tofauti na waandaaji wa kiume wanaonekana wahangaikaji,” alisema.

“Ninatengeneza filamu bila kutegemea nguvu ya mtu yeyote kutoka nje, ndiyo maana nimeweza kufanya kazi zenye ubora ikiwamo ‘Jicho Langu’. Unaweza kujiuliza mambo mengi sana juu ya maneno haya ‘Jicho Langu’. Hii ni filamu iliyoandaliwa chini ya kampuni ya J-Film 4 Life,” alisema Odama.


Alisema ubora wa kazi hiyo unaweza kukuzwa na Watanzania ambao watanunua kopi halali ili kukuza uchumi wa nchi na msanii. “Tatizo tunalokumbana nalo hasa ni wapenzi wa filamu kukimbia kopi halali na badala yake kununua kopi zisizo halali, mwishowe wanawafaidisha watu wengine.”

Hata hivyo, Odama alisema uamuzi alioufanya kwa kuamua kukua kisanii umempa matunda makubwa na kumfanya awe imara katika utayarishaji wa filamu bora wakati wote kwa kutumia kampuni yake ya J-Film 4 Life ambayo inaleta changamoto kwa kampuni nyingine za filamu.
“Ninapofanya kazi nikiwa nimesimama kama Odama kunakuwa na utofauti.Unapokuwa chini ya mtu au kuwa tegemezi , ni vigumu kuwa mwenye ubunifu sana na mwenye mafanikio mazuri.

Comments

Popular posts from this blog