Mashitaka matatu aliyosomewa makamu wa Rais wa Kenya mbele ya mahakama ya ICC


 

William Ruto amekana mashtaka yote yanayomkabili kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). 

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda anayesimamia kesi hiyo, alisema watuhumiwa wawili waliofikishwa mahakamani hapo jana, Ruto na mtangazaji wa Redio, Joshua arap Sang wanakabiliwa na mashtaka matatu kila mmoja, ambayo ni kuwalazimisha watu kukimbia makazi yao, mauaji na kuchochea ghasia.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa siku chache baada ya Bunge la Kenya kupiga kura kutaka nchi hiyo ijitoe uanachama wa ICC, wakieleza kwamba imekuwa haina tija na inatumiwa kuwakandamiza Waafrika.

Comments

Popular posts from this blog