WAZIRI MWAKYEMBE ATUA AIRPORT DSM GHAFLA KUSAKA WAUZA UNGA


Waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe  amefanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere  jijini Dar-es-Salaam na kubaini kuwa upitishwaji wa madawa ya kulevya uwanjani hapo hufanywa kwa msaada wa baadhi ya wafanyakazi    wanaoshirikiana na wasafirishaji hao kupitisha shehena hizo.Waziri Mwakyembe  aliwasili uwanjani hapo majira ya saa kumi na mbili alfajili na kutaka kuonyeshwa hatua ya mwanzo hadi mwisho ya ukaguzi wa mizigo uwanjani hapo na kupokea taarifa toka kwa mamlaka zinazosimamia uwanja huo.

Naye mkurugenzi wa uwanja huo Bw Moses Malaki amesema uwanja unakidhia matakwa ya kiusalama wa kimataifa ila jambo kubwa ni uwepo wa watau wachachae ambo wanafanya kazi kinyume na mfumo huo.
Akihitimisha ziara hiyo Mh Mwakyembe amesema amebaini mambo mengi ikiwemo kuwa katika uwanja huo kuna taasisi nyingi za kiusalama ambazo zinafanya kazi hivyo na kusema kuwa hakuna sababu yeye wala watumishi wengine wa uwanjani huo kuendelea kufanya kazi uwanjani hapo.
Hivi karibuni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa jijini Dar-es-Salaam, uligubikwa na wingu la kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya yaliyo kamatwa nchini Afrika ya kusini yakihusishwa na vijana kutoka Tanzania, jambo lililopelekea Watanzania kukaguliwa ki ziada katika mataifa ya nje ikiwemo Afrika ya kusini hivyo kuchafua jina la Tanzania katika medani ya kimataifa
Chanzo:ITV

Comments

Popular posts from this blog