WAZIRI MKUU WA TANZANIA ASHITAKIWA RASMI....MAWAKILI 19 WAJITOA MHANGA


Kituo cha Sheria na Utetezi wa Haki za Binadamu (LHRC) na Chama Cha Wanasheria Tanzanyika vimefungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama hiyo itoe tafsiri za kisheria katika baadhi ya Ibara.

Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa namba 24 ya mwaka huu, na ambayo bado haijapangiwa jaji, wadaiwa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taasisi hizo ambazo zinatetewa na mawakili wa kujitegemea Harold Sungusia, Francis Stolla na wengine 17, kwa mujibu wa hati yao ya madai, walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya maombi mawili ambayo wanaomba mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika Ibara hizo kwa kuwa wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya mwaka 1977, ambayo 
inaainisha  Haki na Wajibu Muhimu.
  • Wakili Sungusia alilitaja ombi la kwanza kuwa, wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba ya nchi inayotoa  uhuru wa majadiliano kwa wabunge wawapo ndani ya bunge ambayo inasomeka hivi: “kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.”

Wakili Sungusia anadai kuwa Ibara hiyo ina ubaguzi ndani yake kwani inayoa uhuru kwa mbunge kujadili ndani ya bunge na wakati anajadili jambo hata kama amevunja haki za mtu mwingine hataweza kushitakiwa wala kuhojiwa jambo ambalo anadai linakinzana na Ibara ya 13(2) ya Katiba ambapo Ibara hii inasomeka hivi; “ Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake’.

‘...sisi tunaomba mahakama itamke wazi kuwa Ibara ya 100(1) inakwenda kinyume na matakwa ya Ibara 13(2). Zinakinzana, kwa kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba inatoa haki tu kwa upande wa mmoja wa  wabunge uhuru wao kutohojiwa na inawanyima haki ya kuwahoji au kuwashitakiwa wabunge wanaotoa kauli zao bungeni hata kama kauli hizo za wabunge zimevunja haki za wananchi,”alidai wakili Sungusia.

  • Wakili Sungusia alilitaja dai la pili kuwa ni kuiomba mahakama hiyo itamke kuwa kauli ya Waziri Mku, Pinda ambayo ililitaka Jeshi la Polisi kuwapiga wale wote wanaokiuka amri za jeshi hilo, kama kauli hiyo nayo inalindwa na kinga iliyowekwa katika Ibara ya Ibara ya 100(2) ya Katiba ya nchi ambayo inasomeka hivi: ‘Bila  ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya  ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.’

Katiba mkutano wa bunge uliomalizika hivi karibuni , Waziri Mkuu Pinda akiwa ndani ya bunge aliliagiza jeshi la polisi kuwapiga wale wote wanaokaidi amri za jeshi hilo, kwasababu serikali imeshachoshwa na vitendo vya baadhi ya wananchi wanaokaidi kwa makusudi amri za jeshi la polisi , kauli iliyoleta mhemko kwa jamii huku wengine wakiipinga utekelezaji wa agizo hilo na wengine wakiunga mkono, hali iliyosababisha LHRC  hivi karibuni  ilizungumza na waandishi wa habari wakimtaka Pinda afute kauli yake hiyo ama sivyo watamfikisha mahakamani.

Rejea ya habari: Happiness Katabazi, gazeto la TanzaniaDaima  la Ijumaa, Agosti 2 mwaka 2013.

Comments

Popular posts from this blog