KIGOGO WA POLISI ‘AKAMATA’ LORI LENYE SUKARI YA WIZI


-NI RPC WA MKOA WA TEMEKE


Na Makongoro Oging'
NI jambo la kufurahisha kuona kwamba polisi wamekataa rushwa ya shilingi milioni 30 baada ya kuwakamata majambazi waliokuwa wakipakia sukari ya wizi jijini Dar es Salaam.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert I. Kiondo (kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari na maofisa wa polisi shehena ya sukari iliyokamatwa.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita baada ya polisi kukamata magunia 1,312 ya sukari yenye thamani ya shilingi milioni 90.5 yaliyoibwa katika ghala la kuhifadhia bidhaa la Haruni Zacharia Enterprises lililopo Mbagala, wilayani Temeke, Dar.

Polisi hao ambao wako chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Engelbert Kiondo imeelezwa na chanzo chetu kuwa walikataa rushwa hiyo baada ya kuwakamata majambazi 12 wenye silaha za moto na mapanga baada ya kuwakuta laivu wakipakia mifuko ya sukari katika lori la kubebea mizigo.

Kamanda Kiondo akionesha geti la ghala hilo la sukari lililovunjwa na wezi.

Akithibitisha habari hiyo, Kamanda Kiondo alisema ni kweli tukio hilo lilitokea siku hiyo.
“Ilikuwa ni saa mbili usiku ambapo walinzi wanne waliokuwa wakilinda ghala hilo walivamiwa na kufungwa kamba kisha kujeruhiwa kwa mapanga na majambazi kuvunja geti na kuingiza lori, wakapakia sukari,” alisema Kiondo.

Aliongeza kuwa jeshi lake lilifanikiwa kuyanasa majambazi hayo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na baada ya kuwakamata walitaka kutoa rushwa ya shilingi milioni 30 ili waachiwe lakini vijana wake walikataa na kuwafikisha  kituoni.

Kamanda Kiondo akionesha sehemu walipolazwa walinzi katika ghala la Haruni Zacharia Enterprises lililopo Mbagala jijini Dar.
“Nawataka majambazi wote waache shughuli hiyo kwani msako mkali umeanza dhidi yao na nawaomba wananchi waendelee  kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kuwafichua wahalifu wote ili tuishi kwa amani’,”alisema kamanda huyo.CHANZO:GLOBAL PUBLISHER BLOG


Comments

Popular posts from this blog