KAJALA, AUNT, BI MWENDA WAJIKABIDHI WATOTO YATIMA




Kajala Masanja akiwa na mtoto.MASTAA  wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, Kajala Masanja na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ kila mmoja amejikabidhi mtoto yatima ili amlee.
Wasanii hao walijikabidhi watoto hao nyumbani kwa Aunt Ezekiel maeneo ya Mwananyamala jijini Dar, kulipokuwa na shughuli ya futuru hivi karibuni ambapo Aunt aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo watoto hao wa Kituo cha Watoto Yatima, Magomeni.Na Global Publisher

Baada ya kumaliza kufuturu, wasanii hao walijikusanya kwa pamoja na kupiga picha na watoto hao ambapo kila msanii alichagua mtoto wake na kuahidi kwenda kila wakati kumtembelea kituoni na kumpa huduma muhimu kama mwanaye.



Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ naye akiwa na mtoto aliyeahidi kumlea.
Watoto hao walipokuwa wamebebwa na mastaa hao walionekana wenye nyuso za furaha na wakati mwingine walikuwa hawataki kushuka chini wakitaka waendelee kubebwa na mastaa hao.

“Mimi kwa kweli nimefarijika sana kupata mtoto mwingine ambaye atakuwa ni rafiki yangu mkubwa na nitakuwa nakwenda kumtembelea kila wakati na hata hivi leo nilivyofuturu nao ni faraja kubwa sana kwangu kwa vile pia mimi ni yatima,” alisema Aunt Ezekiel.

Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye aliyechagua kumlea.

Comments

Popular posts from this blog