MIRUNGI KILO 50 YAKAMATWA ARUSHA


http://kilimohai.files.wordpress.com/2012/03/fargokhatbust.jpg?w=595
Dawa za Kulevya aina za Mirungi yenye uzito wa Kilo 50 imekamatwa Jijini Arusha baada ya kutelekezwa kwenye gari na watu wasiofahamika.
Duru za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo ACP Liberatus Sabas zimesema Polisi walipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema Julai 24 mwaka huu majira ya saa 6 za mchana maeneo ya Unga Limited Jijini Arusha kuwepo kwa gari linalosambaza dawa za kulevya zilizopigwa marufu nchini aina ya mirungi.
Sabas amelitaja gari lililokamatwa baada ya dereva na waliokuwemo kulitelekeza  na kukimbia kusikojulikana kuwa ni Nissan Wingroad lenye namba za usajili T. 904 BSJ.

Hata hivyo ACP Sabas ametoa wito kwa wananchi kupitia Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kuendelea kutoa ushirikiano pindi matukio ya dawa za kulevya yanapojitokeza katika jamii ili kutokomeza mtandao huo.

Comments

Popular posts from this blog