ANGALIA PICHA ZA MBOWE AKIZINDUA KANDA YA KUSINI



 
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akiingia katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea ili kuzungumza na wananchi.



Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akihutubia wananchi jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini uliofanyika katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea.
Wananchi wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe  wakati  akihutubia wananchi katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea jana.
Kila mtu alijitahidi kupata nafasi nzuri ili aweze kufuatiliwa vyema matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huu kama inavyoonekana.

Njiwa walirushwa kuonesha ishara ya upendo wakati wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini ya Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Mwenyekiti CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akihutubia wanachama wa CHADEMA katika mkutano wa kuchagua viongozi wa chama Kanda ya Kusini ya mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage mjini Songea.
Mwenyekiti wa taifa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi Mwenyekiti mteule wa CHADEMA Kanda ya Kusini katiba ya CHADEMA ambayo atapaswa kuilinda na kuitetea wakati wa uongozi wake.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kusini, Mwalimu Joseph Matiko akizungumza katika mkutano wa wanachama wa CHADEMA kanda ya kusini (hawapo pichani) ambapo aliwashukuru kwa kumchagua na akaahidi kuitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Kushoto ni Makamu mwenyekiti kanda ya kusini Lusajo Mwangupili.



Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimtakia kila la heri Mwenyekiti wa kanda ya Kusini Joseph Matiko. Kushoto ni Makamu mwenyekiti kanda ya kusini Lusajo Mwangupili.

Mwananchi mmoja, aliyejitambulisha kw a jina laWilly Migodela (Kulia), akiwasomea wananchi kipengele cha mwaka 2006 katika katiba ya CHADEMA kuhusu  uhalali na wajibu wa vikundi vya Red Brigade katika chama kikatiba.
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi Kanda ya kusini uliofanyika mjini Songea jana.

 
Viongozi mbalimbali wakitoa salam kwa wananchi wakati katika mkutano wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini ya mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma uliofanyika katika viwanja vya Stendi ya Malori mjini Songea.

Comments

Popular posts from this blog