Posts

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
 

Breaking News….Darassa Apata Ajali Kahama Mkoani Shinyanga

Image
Muonekano wa gari alilopata nalo ajali ainaya Toyota Harrier Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye anasumbua na ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif  Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier  ambalo dereva hajajulikana, Darassa alikuwa ameambatana na director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo na alipopigiwa simu na Global Publishers  alisema hawezi kuongea kwa sasa hivyo atafutwe baadaye.

Penzi la Jide, Nusu Bongo, Nusu Nigeria

Image
Mpenzi wa Jide, Spicy naye akifunguka mbele ya kamera za Global TV Online. BAADA ya kukaa muda mrefu bila kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash, hivi karibuni mwanamuziki nguli wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ aliamua kumuanika mchana kweupe mpenzi wake mwingine aitwaye Spicy. Mwanamuziki huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, siku hizi za usoni baada ya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria, ameonekana ni mtu mwenye furaha na asiyeweza kuficha hisia zake za mapenzi ya kweli kwa mwenza wake huyo. Mapema wiki hii, Jide aliibuka ndani ya mjengo wa Global Publishers akiwa ameambatana na Spicy, mambo yakawa hivi mbele ya waandishi wa Global TV. Wapenzi hao wakifurahia jambo wakati wa mahojiano na Global TV Online. Amefika na je hakuna machozi tena? “Unajua hata kama nilikuwa naimba nyimbo nyingi zinahusiana na mambo ya kutendwa kimapenzi lakini ukweli nil