Posts

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA HALMASHAURI YA ARUSHA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majliwa

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 15.12.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo Akamatwa na Polisi, Anyimwa Dhamana

Image
  DAR ES SALAAM: Mwanzilishi, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa selo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Police Central) leo Desemba 13, 2016. Polisi wameeleza muda huu kwamba leo atalala ndani (selo) hadi kesho atakapofikishwa mahakamani. Imeelezwa kuwa, kosa la kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni kukataa kutoa taarifa binafsi zilizohitajika za wateja wa mtandao anaoumiliki wa JamiiForums. Maxence ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa, kufanya hivyo ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi. Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari. CHANZO: JAMII FORUMS

MSANII CHUCHU HANS ASEMA HAYA BAADA YA KUSHINDA TUZO

Image
  Ushindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike wa Tuzo za EATV 2016 kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha mambo mengi aliyopitia kwenye maisha yake. Muigizaji huyo ambaye hakuwepo kwenye usiku huo wa tuzo na kuwakilishwa na meneja wake, ametoa ya moyoni kupitia Instagram kwa kusema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake. “Naamini kuna uwepo wangu kwa kila hatua tupigayo, ama hakika usitamalaki ya moyoni kwa kuyadhihaki ya machoni. Hii imenipa funzo zaidi ya lile alilonipa mama nikiwa na vunja ungo,” alisema Chuchu. “Mama aliniambia heshimu watu bila kuwa dhihaki kwa makundi,ama kuwa bagua kwa rika,” “Niwashukuru wote mlio nipigia kura amahakika mme tenda vema,likini mimi sio bora kuliko wenzangu ila nadhani kwa wino wakura zenu ulistahili niwe BEST ACTRESS, niwashukuru zaidi na zaidi, nikiandika maneno haya machozi yananitoka lakini hii yote ni heshima mlio nivika NENO LA KALE NI ASANTE,” aliongez

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Alichokisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kwenye Sherehe za Maulid, Singida

Image
Katika kusherekea siku ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammed (S.A.W), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali imani zao za kidini. Majaliwa ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida na kusema kuwa kuna matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika jamii na katika kuyachukulia hatua za kisheria vitendo hivyo Serikali haitakuwa ikibagua mtu kutokana na imani yake ya kidini kama jinsi inavyofanya kwa shughuli za maendeleo. “Serikali inawashukuru sana kwa kuendelea kuunga mkono jitihada ya Serikali ya Rais Magufuli, tunaamini juhudi tunazofanya za kuweka nidhamu kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi mtaendelea kutuunga mkono, tutaendelea kuruhusu uhuru wa kuabudu na kushirikiana na viongozi wa dini lakini tu mafundisho yanayotolewa yasikiuke sheria na kanuni za nchi, “Serikali ipo macho kupambana na tukio lolote lenye nia ya kupoteza amani ya

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. “Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema. “Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi

Meli Yenye Malori 600 ya Kiwanda cha Dangote Yawasili Mtwara

Image
MTWARA: Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dangote Cement Industries ya jijini Mtwara, ambaye pia ni bilionea namba moja Barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote jana Desemba 10, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini. Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana kuwa meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake mikoani, itawasili nchini. Aliongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini. Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo. Aidha, imeelezwa kuwa w