UZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI NI KESHO VIWANJA VYA MWEMBE YANGA JIJINI DAR ES SALAAM MAANDALIZI YAMEKAMILIKA WANA MUZIKI LULUKI KUTOA BURUDANI WANDUGU SAIDIA TUTANI UZINDUZI RASMI NI KESHO
Mshauri wa masuala ya Malaria kutoka Taasisi ya Jhpiego, Jasmin Chadewa (kushoto), akitoa huduma ya kumpa dawa ya vitamini A, mtoto Rahim Simai, viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi ikiwa ni utoaji huduma wa elimu ya afya kwa wajawazito na matumizi ya dawa aina ya SP, upimaji wa malaria pamoja na matumizi ya vyandarua kama muendelezo wa huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika kesho katika viwanja hivyo. Wakina mama wakisubiri kupata huduma katika moja ya banda yaliyopo viwanja vya Mwembe Yanga. Maofisa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University wakifunga kitanda cha kujifungulia wajawazito wakati wakitoa huduma mbalimbali viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi tayari kwa uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika katika viwanja hivyo kesho. Mtaalamu wa Maabara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mbwan