Jinsi ya kuruka vihunzi vya mwanume anayekutongoza mara kwa mara
Miongoni mwa kero ambazo huwakumbuka wadada wengi ni pamoja na kutongozwa, jambo hili huwa halikwepeki kwani lipo tu. Hivyo kama wewe ni msichana ambaye upo kwenye mahusiano na bado unaendelea kukutana na ushawishi wa kutongozwa kila iitwapo leo pindi ukutapokutana na mtu ambaye anakutongoza unatakiwa kuwa hivi. 1. Usijibu mtu huyo simu wala texts zake. Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamulingani. 2. Mblock katika mitandao ya kijamii. Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mb...