Utapeli mkubwa waibuka 40 ya Mzee Majuto
AMA KWELI kufa kufaana! Hayo ndiyo maneno unayoweza kusema endapo yatakufikia madai ya utapeli mzito unaofanywa na baadhi ya watu wakiwemo wasanii wa kuchangisha pesa kinyume na taratibu wakidai eti ni kwa ajili ya kufanikisha 40 ya marehemu Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Taarifa hiyo ya kushtua ilipenyezwa na mmoja wa wasanii wa komedi Bongo, Jabir Ally ‘Wajajo’ ambaye alidai kuwa, akiwa katika mishemishe zake Mitaa ya Kariakoo jijini Dar alikumbana na baadhi ya wafanyabiashara waliohoji juu ya uhalali wa watu hao kuchangisha michango ya 40 hiyo. Alisema: “Kuna jambo la kushangaza sana nimekutana nalo huku Kariakoo, kuna watu wanapita kwenye maduka na kuomba michango ya kufanikisha 40 ya Mzee Majuto, mimi sikuwa na taarifa ya utaratibu huo, nikahisi kuna utapeli unafanyika. “Lakini katika kufuatilia nikagundua yupo pia msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Majuto, Bi Rehema, naye anapita kuomba michango, nilipomuuliz