DAR ES SALAAM: Maandalizi ya pati ya kuzaliwa (birthday) ya bintiye ambaye ndiye uzao wake wa kwanza, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ (3), yamemfanya baba’ke ambaye ni staa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa kiapo kizito kuwa itakuwa ni shughuli ya kufuru, Risasi Jumamosi linakupa exclussive. Agosti 6, mwaka huu, Tiffah atatimiza umri wa miaka mitatu tangu alipozaliwa Agosti 6, 2015, lakini sherehe hiyo imesogezwa mbele ambapo sasa itafanyika Agosti 17 hadi Agosti 20, mwaka huu. DIAMOND NA RISASI JUMAMOSI Akizungumza na Risasi Jumamosi juu ya pati hiyo ya Tiffah ya kutimiza umri wa miaka mitatu, Diamond alisema kuwa, yupo tayari kufilisika, lakini ahakikishe mwanaye huyo ana furaha kwa kumfanyia pati hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria. “Nimepanga iwe sherehe kubwa sana, acha nifilisike, lakini mwanangu afurahi,” ndivyo alivyoanza Diamond kwenye mahojiano hayo maalum na Risasi Jumamosi na kuongeza: “Nipo tayari kutumia sehemu ya pesa za...