Posts

BETHIDEI YA TIFFAH KUFURU

Image
DAR ES SALAAM: Maandalizi ya pati ya kuzaliwa (birthday) ya bintiye ambaye ndiye uzao wake wa kwanza, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ (3), yamemfanya baba’ke ambaye ni staa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa kiapo kizito kuwa itakuwa ni shughuli ya kufuru, Risasi Jumamosi linakupa exclussive. Agosti 6, mwaka huu, Tiffah atatimiza umri wa miaka mitatu tangu alipozaliwa Agosti 6, 2015, lakini sherehe hiyo imesogezwa mbele ambapo sasa itafanyika Agosti 17 hadi Agosti 20, mwaka huu. DIAMOND NA RISASI JUMAMOSI Akizungumza na Risasi Jumamosi juu ya pati hiyo ya Tiffah ya kutimiza umri wa miaka mitatu, Diamond alisema kuwa, yupo tayari kufilisika, lakini ahakikishe mwanaye huyo ana furaha kwa kumfanyia pati hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria. “Nimepanga iwe sherehe kubwa sana, acha nifilisike, lakini mwanangu afurahi,” ndivyo alivyoanza Diamond kwenye mahojiano hayo maalum na Risasi Jumamosi na kuongeza: “Nipo tayari kutumia sehemu ya pesa za...

TAGCO NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZAPONGEZWA KWA UTENDAJI

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza kuhusu namna Halmashuri hiyo ilivyojipanga katika kuimarisha mawasiliano ya kikakati hasa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea  Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao. Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamo...

WAZEE WA NITUMIE PESA KWA NAMBA HII’… WANASWA

Image
I RINGA: Yawezekana wewe ni kati ya watu ambao walishawahi kutumiwa meseji za kitapeli kutoka kwa watu hao (pichani) ambao huandika hivi; ‘ile pesa nitumie kwenye namba hii, jina litatokea…, simu yangu ina tatizo’. Kama jibu ni ndiyo basi habari ikufikie kwamba, watuhumiwa wengine wapatao saba wa utapeli huo hivi karibuni wamenaswa mkoani Iringa baada ya kuwaliza watu wengi kwa muda mrefu. Watu hao wamekuwa wakiwatumia watu meseji na kuwaelekeza kuwa watume pesa, mazingira ambayo baadhi huenda walikuwa na watu ambao ilikuwa wawatumie pesa hivyo hutuma na kujikuta wametuma kwa matapeli hao. POLISI WATANGAZA VITA Kufuatia kushamiri kwa utapeli huo katika mikoa mbalimbali, jeshi la polisi kupitia kwa makamanda wa mikoa hivi karibuni lilitangaza vita dhidi ya uhalifu huo na kufanikiwa kuwanasa baadhi ya watu huku tahadhari ikitolewa kwa wananchi kuwa makini wanapokumbana na meseji za aina hiyo. WALIONASWA IRINGA Mbali na wale 15 wa hivi karibuni waliokamatw...

MWANAMKE KUKOSA MSISIMKO WA TENDO LA NDOA

Image
T ATIZO hili la mwanamke kukosa msisimko wa tendo la ndoa kitaalamu tunaita ‘Female Sexual arousal disorder’. Mwanamke akiwa na hali hii huwa hajihisi hamu wala haja ya kuhitaji tendo hilo na wakati mwingine huona kama usumbufu endapo atakuwa katika mahusiano. Mwanamke wa aina hii kama yupo mwenyewe au ‘single’ haoni umuhimu wa kuwa na mpenzi au mwenza na hasa kama anajimudu kiuchumi. Wapo baadhi ya wanawake wenye hali hii ambao hawana watoto au wengine wanamtoto mmoja au zaidi na aidha wameachana na wenza wao au wenza wao walishafariki. Msisimko hupatikana baada ya hamu ya tendo la kujamiiana kuwa juu ya kiwango na kusababisha mabadiliko mwilini na kusaidia mwili uwetayari kwa tendo. Hali ya msisimko kwa mwanamke haina tofauti na hali ya mwanaume kusimamisha uume wake. Mwanamke aliyepoteza msisimko huwa hajisikii chochote wakati wa ’ Romance’ au maandalizi ya tendo la ndoa, wengine huwa hawapati hamu na wengine hupata hamu kwa kiasi kidogo lakini hawapati mguso au ...

Diamond azuiwa na Basata kwenda kufanya shoo nje

Image
BARAZA la  Sanaa Tanzania (BASATA) leo limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali. Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Onesmo Mabuye alipokuwa akizungumza na TBC, kuhusiana na sintofahamu hiyo kuwa ni kutokana na msanii huyo kukosakibali cha Basata. BASATA wamesema kwa sasa hivi kuna utaratibu mpya ni kuwa msanii akitaka kwenda kufanya shoo nje ya nchi ni lazima apitie kwa BASATA wampe kibali na kisha akirudi pia anatakiwa kuripoti kwao BASATA wamesema kumzuia Diamond wanataka iwe fundisho kwa wasanii wengine ili wanapoenda nje ya nchi wafuate taratibu zilizowekwa.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU AGAWA BAISKELI KWA WALEMAVU

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge wanaoishi katika mazingira magumu. Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,Nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga. Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa ...

Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika

Image
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaz...

Zari Awapiga Stop Wema, Aunt: Sitaki Kunichafulia Nyumba, Kaeni Hukohuko

Image
IKIWA ni saa chache baada ya mwanamuziki Diamond Platnumz kualika watu takribani 50 kuuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mtoto wake  Tiffah, mzazi mwenzake, Zari Hassan amepiga marufuku ugeni huo. Jana wakati wa sherehe ya kufikisha siku 40 ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema, Diamond alialika wanakamati zaidi ya 10 kuhudhuria sherehe hiyo ya Tiffah, Sauzi hukuakisema atalipia tiketi za watu 30 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe na kuwalipia watoto 10 na wazazi wao. Hata hivyo, Zari amemjibu kupitia mtandao wa Instagram aliandika kuwa hautaki ugeni huo akihofia kuchafuliwa nyumba yake:  “Sitaki kunichafulia nyumba kaeni hukohuko.” Miongoni mwa wanakamati walioalikwa ni Wema Sepetu ambaye amewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz na mwigizaji Aunty Ezekiel. Tiffah ambaye jina lake halisi Latiffah alizaliwa Agosti 6, 2015. Hata hivyo sherehe za kuzaliwa binti huyo zitafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 17- 19 mwaka huu.

Katibu Tawala Mkoa Mtwara wa Awaasa Maafisa Habari Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Weledi

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa  Mwakililishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya  kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika mkoa huo. kurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara  Bw. Omari Kipanga akisisitiza jambo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya  kuziondoa hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma kat...

HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAJIDHATITI KUIMARISHA MAWASILIANO NA WANANCHI

Image
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO  Bi. Gaudensia  Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi.  Changwa Mkwazu      wakati wa ziara ya ujumbe huo katika halmashauri hiyo uliolenga kuona utendaji kazi wa Maafisa  Habari na Mawasiliano na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuisemea Serikali kimkakati. Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Bi mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya  ujumbe  wa viongozi wa Chama cha ...

Nyumba mbili zachomwa Moto Mwanza kisa wizi

Image
Na Paschal D.Lucas, Mwanza Wananchi waliojichukulia sheria mkono wamechoma nyumba mbili za familia moja na nyingine kuziharibu katika mtaa wa Nyakabungo "A" kata ya Isamilo wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  baada ya kuona watoto wa familia zile wanajihusisha na uhalifu hapo mtaani hapo mara kwa mara. Maamuzi hayo yamekuja baada ya wananchi kudai kuwa watoto hao wamekuwa wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kushitakiwa lakini mara nyingi wamekuwa wakiachiwa kwa dhamana na kurudi mtaani kuendelea tena na tabia hiyo kitendo ambacho kimekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 usiku wa tarehe 25,Julai 2018 ambapo katika tukio hilo nyumba mbili zilizoharibiwa ni mali ya Selina Francis (50) na Abdallah Mwita wote wakiwa ni wakazi wa Nyakabungo mkoani humo. Vile vile nyumba moja mali ya Manka Francis James iliharibiwa vibaya na kundi hilo kwa kuvunjwa milango na madirisha na kuharibu vitu mbalimbali vilivyokuwemo ndan...

Tambwe Afunguka Mazito Yanga

Image
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya ku­fungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya. Akizungumza na Championi Jumatano , Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa maru­diano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti. “Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitege­mea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata ma­tokeo. “Nadhani huu ni wakati wa kuende­lea kushikamana, mashabiki wetu hawa­paswi kuendelea kuka...

Mbelgiji Aanza Kukiunga Kikosi Upya

Image
KOCHA Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameanza kutoa mafunzo ya mfumo anaotaka kuutumia katika msimu wa 2018/19 akiwa na Simba. Simba imeweka kambi ka­tika mji mdogo wa Kartepe ambao uko mlimani kabisa, sehemu maalum kwa ajili ya kambi za timu. Aussems ameanza kukinoa kikosi chache akiwafundisha mifumo na namna ya uchezaji katika masuala mbalimbali. Kocha huyo amekuwa aki­waonyesha wachezaji wake namna ya kulinda lakini pia kushambulia kwa tahadhari. Wakati Simba ilipotua hapa, kocha huyo alianza kutoa mafunzo ya kawaida, zaidi wachezaji wakioneka­na kupasha misuli kawaida. Inaonekana ame­kuwa akiongeza mazoezi taratibu huku akichanganya na aina ya uche­zaji. Makocha wengi huanza kufundisha mifumo baada ya timu zao kupata mazoezi ya kuto­sha. Lakini Mbelgiji huyo anaonekana kuwa tofauti ki­dogo akienda anachangan­ya mazoezi ya kawaida na mifumo, taratibu.

Beki Simba atua Singida United kwa mkopo

Image
Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kuwa imemsajili mchezaji Jamaly Mwambeleko kutoka Simba kwa usajili kamili tofauti na taarifa zilizoeleza kuwa wamemchukua kwa mkopo, huku wakiweka wazi kuwa wamemwongeza mwaka mmoja na sasa ni mchezaji wao kwa miaka miwili. Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameeleza kuwa walifanya mazungumzo na Simba na kumalizana nao kisha kumpa mkataba wa mwaka mmoja Jamaly Mwambeleko lakini baadae walimwongeza mwaka mmoja na kuwa miwili. ''Tumemsajili Mwambeleko kwa usajili kamili wala hajaja kwetu kwa mkopo, ila awali mazungumzo yalikuwa hivyo lakini kocha Hemed Morocco akapendekeza tuwe naye kwa muda mrefu ndio akasaini mkataba wa kuitumikia Singida United kwa miaka miwili'', - amesema. Jamaly Mwambeleko ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kushoto ni sehemu ya wachezaji walioachwa na Simba katika usajili huu kwa kile kilichoelezwa ni kutokuwa na nafasi ya kucheza hususani nafasi yake pale Simba kuwa na w...

Jafo azitaka halmashauri kutoweka riba mikopo ya wajasiriamali

Image
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo amezitaka halmashauri za miji na majiji kutoweka riba katika fedha za mikopo zinatolewa kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali hapa nchini. Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 950 zilizotolewa na jiji la Dodoma kwa wajasiliamali, Mheshimiwa Jafo amesema serikali ya awamu ya tano inalenga kuwawezesha watanzania hivyo haikubali wananchi kutozwa riba. Akizungumza katika tukio hilo, naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,ajira kazi vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesema jiji la Dodoma ni kati ya halmashauri chache nchini zilizoweza kutimiza sheria ya kuhakikisha linatoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu ili Kuwawezesha kuondokana na umaskini. Akielezea kuhusu fedha hizo, mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi amesema jiji la Dodoma limevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka...

KINDA WA LEICESTER CITY AITWA SERENGETI BOYS KUCHEZA MICHUANO YA CECAFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemualika mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Leicester City ya England, Anthony Starkie kuja kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. Taarifa ya TFF usiku wa Jumatano imesema kwamba Starkie anatarajiwa kuwasili Alhamisi mjini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa na Leicester City, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya wakubwa England. Atajiunga na Serengeti Boys ambayo inajiandaa kushiriki michuano maalum ya vijana Afrika Mashariki na Katik ijulikanayo kama CECAFA Zonal Qualification. Wazi uamuzi wa TFF kumuita kijana huyo unafuatia agizo la Mkurugenzi wa Michezo, Dk. Yusuphu Singo kwamba wafuatilie vipaji vya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje. Singo alitoa kauli hiyo kufuatia mshambuliaji Yussuf Yurary Poulsen, anayezaliwa na baba kutoka Tanga  kuichezea Denmark, nchi ya mama yake kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchi...

Makamu wa Rais aahidi Serikali kutatua changamoto ya barabara Mbeya

Image
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba serikali imejipanga kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu ya barabara. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya eneo linalotajwa kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.  Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40 ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).  “Mwaka juzi mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema. Mama Samia pia amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa...

BREAKING: SANGA ATANGAZA RASMI KUACHIA NGAZI YANGA

Image
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo. Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri. Kiongozi huyo aliyekuwa akikaimu nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, alikuwa akitupiwa lawama na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Khalfan Hamis ambaye amejiuzulu juzi akidai Sanga amekuwa si mweledi wa mambo. Mbali na kukosa maelewano, Sanga ameeleza kuwa kuna CLIP ameiona mitandaoni inayohamasisha watu kumvamia kwa mapanga ni moja ya sababu zilizopelekea kufanya uamuzi wa kuachia ngazi. Aidha,wiki kadhaa zilizopita Mjumbe mwingine kutoka kamati hiyo, Salum Mkemi naye aling’atuka kuendelea na wadhifa huo ndani ya Yanga na akisalia kuwa mwanachama pekee kutokana na kutokuwa na kukosa maelewano mazuri baina yake na wanachama wa klabu. Ukiachana na Sanga, Kati...

Rais Magufulia atoa agizo kwa Mkandarasi Daraja la Salender

Image
Rais John Magufuli amemuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi wa kujenga daraja kubwa la Selander Bridge kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan litakalogharimu shilingi bilioni 250 kwa ufadhili wa Serikali ya Korea kusini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ndani ya miezi 36 aliyopangiwa  kufanya kazi. Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kushuhudia mkataba wa utiaji saini ujenzi wa darala hilo ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 6.23 mbele ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini Mh.0 Lee Nak-Y eon Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutaendelea kubadilisha taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam katika miundombinu ya barabara. Katika tukio jingine, hivi sasa Rais Magufuli anapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.

Tanga: Diwani wa CUF Avuliwa Udiwani kwa Kutofika Vikaoni

Image
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imemuondoa kwenye nafasi yake, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mussa Mbarouk,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, baada ya kupoteza sifa kwa kutohudhuria vikao sita mfululizo. Kata hiyo sasa imetangazwa kuwa wazi. You May Like