Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaz