KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,SANAA UTAMADUNI NA MICHEZOAMTEMBELEA MWANARIADHA ANAYEHESHIMIKA DUNIANI MZEE JOHN STEVEN AKHWARI NYUMBANI KWAKE MBULU MKOANI MANYARA
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sani mjini Mbulu mkoani Manyara jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Mexco City mwaka 1968 John Steven Akwari aliyekuwa wa mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008 katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye, Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya 75 walioanza. Mshindi wa mashindano hayo Mamo Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya saa moja baadaye yaani alitumia