Posts

Zari Amlilia Masogange, Akumbuka SMS Zake

Image
Video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’ enzi za uhai wake. MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, kupitia akaunti yake ya Snapchat. Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia Mtandao wa Snapchat Zari ameandika; We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis.

Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani rahisi Kutumia

Image
       Kipimo cha mimba cha nyumbani ni rahisi sana kukitumia wewe mwenyewe kwa wakati wako ikiwa unajihisi umjamzito au kuhisi mwenzi wako ana ujauzito. Unachotakiwa kuwa nacho ni moja, Kipimo hichob‘Pregnancy Test’ ambacho kinapatikana katika maduka yote ya madawa ya Binadamu, na pili mkojo wa anahisiwa au kuhisi ana mimba. mara nyingi ni rahisi zaidi kupata majibu ya uhakika ukitumia mkojo wa kwanza kabisa asubuhi kisha uweka kwenye kikopo kidogo na kisha fuata maelekezo ya kwenye picha hii:- Hatua; 1.    Fungua pakiti iliyo na kipimo cha mimba. 2.    Tofautisha sehemu ya kushika na sehemu utakayotumbukiza kwenye kikopo chenye mkojo. 3.    Acha kwa dakika zipatazo 3, bila kuzidisha sehemu yenye mstari uliyoandikwa MAX. 4.     Toa na kisha soma majibu yaliotokea. Majibu yatatoka kama ilivyo katika picha hii inayofuata ya vipimo viwili tofauti vilivyofanyiwa majari...

Siri 6 Kiba Kumuoa Mkenya Zaanikwa!

Image
Ali Saleh Kiba ‘King Kiba akiwa na Mkewe Amina N YUMA ya tukio kubwa na la kihistoria kwenye ulimwengu wa burudani, lililogubikwa na kufuru ya fedha la staa wa Bongo Fleva wa Afrika Mashariki, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kumuoa mrembo mkali kutoka Mombasa nchini Kenya, kuna siri sita (6), Risasi Jumamosi linazianika.  Juzi alfajiri ya Aprili 19, mwaka huu, Kiba alifunga ndoa na mrembo Amina Khaleef katika Msikiti wa Ummul Kulthum uliopo mjini Mombasa, Kenya. Ndoa hiyo ilifungishwa na Sheikh Mohamed Kagera. Hakika ilikuwa ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi hao, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mjini Mombasa mara baada ya ndoa hiyo kufungwa. Mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, mitandaoni kulichafuka ambapo baadhi ya mashabiki wa Kiba walikuwa wakihoji ni kwa nini mkali huyo wa Wimbo wa Seduce Me ameacha warembo kibao Bongo na kwenda kwa Amina wa Mombasa? Kufuatia wengi kutaka kujua Amina ni nani au ana nini cha tofauti kilichomteka Kib...

Kajala amkimbiza mke wa P Funk

Image
   Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amedaiwa kusababisha mke wa prodyuza mahiri Bongo, Paul Matthysse, Samira afungashe virago vyake tayari kwa kurudi kwao. Mke huyo wa P Funk amedaiwa kufikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kuonekana kurudisha majeshi kiaina kwa Kajala aliyewahi kuwa mchumba’ke zamani huku picha na video mbalimbali za kimalovee zikivuja. Mtu wa karibu na mke wa P Funk alivujisha kuwa, Samira amefikia hatua hiyo baada ya kushuhudia matukio mbalimbali ya P Funk na Kajala na kukosa majibu yaliyonyooka. “Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala. “Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala,” alidai mtu huyo wa karibu. Akizidi kushusha data, mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akie...

TCRA Yaanza Rasmi Usajili wa Blogu, Redio na TV za Mtandaoni

Image
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetangaza kuanza rasmi zoezi la usajili wa wamiliki wa Blogu, Majukwaa ya Mtandaoni (Online Forums), Redio pamoja na Televisheni za mtandaoni kuanzia leo Jumamosi, Aprili 21, 2018 kwa mujibu wa sheria.

Masogange kuagwa Leaders, kuzikwa nyumbani kwa.

Image
Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao jijini Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko. Akizungumza na www.eatv.tv dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes  utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders,  na kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi “Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald. Sambamba na  hilo muigizaji Steve Nyerere ambaye yuko karibu na familia ya Agnes amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi leaders jioni ya leo, ili kujadili utaratibu wa mazishi na mengineyo. Agnes Masogange amefariki jana April 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pneumonia

NDOA YA KIBA YAACHA VILIO!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ akitarajiwa kuangusha bonge la sherehe baada ya kufunga ndoa nchini Kenya, ndoa hiyo imedaiwa kuacha vilio vikali kwa wanawake ambao waliwahi kushea kitanda na msanii huyo, Ijumaa lina mchapo kamili. Kiba alitarajiwa kufunga ndoa hiyo jana mjini Mombasa nchini Kenya kisha kufuatiwa na bonge la sherehe mjini humo huku sherehe nyingine bab’kubwa ikitarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwezi huu. MTU WA KIBA ANENA Mtu wa karibu na AliKiba, amepenyeza habari kuwa, licha ya kwamba wao wanasherehekea harusi ya mkali huyo anayetamba na Wimbo wa Seduce Me, nyuma yake kuna vilio vingi kutoka kwa wanawake ambao walitembea na Kiba kabla. “Kama unavyojua Kiba alishazaa watoto wanne, wale watoto kila mmoja ana mama yake. Sasa mama zao wanalia maana nao walikuwa wana matarajio ya kuolewa,” alisema mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina na kuongeza: BIBI HARUSI NJIA PANDA “Kimsingi wamem...

Wenger Aondoka Rasmi Arsenal

Image
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameridhia kubwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu baada ya majadiliano ya kina na uongozi wa klabu hiyo kongwe duniani. “Baada ya kutafakari kwa kina kufuatia mazungumzo na klabu yangu, u mefika wakati sasa nikae pembeni mwisho wa msimu huu, nina furaha sana kwa muda wote niliokaa hapa klabuni. “Ninawashukuru wafanyakazi wenzangu, wachezaji, wakurugenzi na mashabiki kwa kuifanya klabu hii kuwa spesho, nimeitumikia kwa miaka mingi” amesema Wenger kwenye taarifa yake rasmi leo Ijumaa. LONDON, England.

Breaking News: Masogange Afariki Dunia

Image
Video queen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde (leo Aprili 20, 2018) katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.  Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kupelekwa Muhimbili kuhifadhiwa. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu. Global Publishers imefika hospitalini hapo na kujionea umati wa watu waliokusanyika wakilia kwa uchungu kumpoteza msanii huyo. Dkt. Kihama Ngoma ameithibitishia Global Publishers na kusema taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Tayari mwili wa marehemu Masogange umehaimshwa hospitalini hapo na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, AMEN!.

Mfalme Mswati III Abadili Jina la Nchi Yake

Image
MFALME Mswati wa III wa Swaziland amebadilisha jina rasmi la taifa hilo kutoka Swaziland na kuliita Ufalme wa eSwatini (The Kingdom of Swaziland)  wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 50 na wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka 50 ya uhuru wake. Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa III kwa miaka mingi. eSwati ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 na katika ufunguzi wa bunge la nchini mwake mwaka 2014. Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki na ametawala tangu mwaka 1986.  Mswati III kwa sasa ana wake 15 akiwa anaifuata rekodi ya Baba yake aliyekuwa na wake 125. Wanaharakati wa kutetea usawa wa jinsia wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa kushangaza na unawabagua wanawake. Mswati III ametoa sababu kuu ya kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aenda...

Siwa ya Bunge yakutwa kwenye Flyover

Image
Baada ya watu wenye silaha kuvamia Bunge la Senate la Nigeria na kuiba siwa juzi, hatimaye imekutwa chini ya Barabara ya Juu ‘flyover’ Jijini Abuja baada ya kuonwa na mwananchi aliyekuwa akipita maeneo hayo. Inadaiwa watu hao waliongozwa na Mbunge Ovie Omo-Agege ambaye amefungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na tuhuma hizo. Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ya Nigeria ameeleza kuwa kitendo hicho ni uhaini na inaashiria kuwa mtuhumiwa, Omo-Agege alikuwa akijaribu kupindua moja ya mihimili ya Serikali ya Nigeria. Siwa ni ishara ya mamlaka ya Bunge hilo na Sheria haziwezi kupitishwa bila kuwepo kwa kifaa hicho. Licha ya kitendo hicho, Bunge liliendelea na kazi yake kwa kutumia Siwa ya ziada iliyokuwepo bungeni hapo ambapo kabla ya hapo Seneta wa Kaduna, Shehu Sani alivua mkanda wake na kuuweka sehemu ya Siwa hiyo. Aidha, Chama tawala, APC kimeita tukio hilo kuwa ni shambulio kwa Demokrasia ya nchi hiyo na kutaka waliohusika kukamatwa. Hadi sasa Seneta Omo-...

SHUHUDIA UKUMBI WA HARUSI YA ALIKIBA NA AMINA UNAVYOWAKA

Image
BAADA ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ kufunga ndoa na mchumba wake, Amina Khaleef Mjini Mombasa nchini Kenya leo, Aprili 19, 2018, sherehe ya harusi ya msanii huyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mombasa. Kiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu wa msanii huyo. Kiba amesema ameamua kufunga ndoa yake siku ya leo kwani siku kama hii ndiyo wazazi wake walifunga ndoa yao miaka kadhaa iliyopita.  

BABU SEYA, FAMILIA YAKE WATINGA BUNGENI – PICHA

Image
MWANAMUZIKI nguli wa dansi,  Nguza Viking ‘Babu Seya’  na watoto wake ambao ni  Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza , leo Alhamisi, Aprili 19, 2018 wametembelea  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma  baada ya kualikwa na  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile. Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai,   baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo. Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.

REKODI 3 NDOA YA KIBA!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ amefunga ndoa leo pande za Mombasa nchini Kenya, nyumbani kwa bibi harusi, Amina Khaleef, imeelezwa kuwa ndoa hiyo inatarajia kuandika rekodi ya mambo makubwa matatu. Akizungumza na Gazeti la Amani, mmoja wa mameneja wa mwanamuziki huyo, Aidan Sefu, alisema tayari wamelipwa mamilioni ya fedha na moja ya luninga ya hapa Tanzania kurekodi na kurusha live harusi hiyo.“Itakuwa kitu kikubwa sana, ni harusi ya aina yake hivyo nisingependa kuongea sana lakini watu wataona,” alisema Aidan. Kama hiyo haitoshi, Amani lilielezwa kuwa miongoni mwa rekodi zinazotarajiwa kuandikwa katika harusi hiyo ni pamoja na kukodiwa ndege maalumu ya kwenda Mombasa na kurudi Bongo. “Kutakuwa na utofauti mkubwa kwani Ali anatarajiwa kukodi ndege kumpeleka kama bwana harusi na ndege ya kumrudisha akiwa tayari na kifaa chake ili kuja kumalizia sherehe huku mwisho wa mwezi,” alisema mnyetishaji wetu. Pia mnyetishaji huyo alisema rekod...

SHUGHULI YA NDOA YA ALIKIBA IMEANZA KENYA – Picha

Image
ILE siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kushuhudia ndoa ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ hatimaye imewadia na leo Aprili 19, 2018 mkali huyo anafunga ndoa yake na mrembo Aminah Rikesh Khaleef mjini Mombasa nchini Kenya. Tayari wapenzi hao wanaofunga ndoa, Mashehe, ndugu na marafaiki wameshafika eneo ambapo ndoa hiyo inafungwa na tayari shughuli imeshaanza kama picha zinavyoonyesha. Watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo. Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine. Tazama video ushuhudie mwenyewe.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa watu 10

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 18, 2018 ameteuwa watu kumi kushika nafasi mbalimbali akiwepo Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanza April 17, 2018