Posts

NDOA YA KIBA YAACHA VILIO!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ akitarajiwa kuangusha bonge la sherehe baada ya kufunga ndoa nchini Kenya, ndoa hiyo imedaiwa kuacha vilio vikali kwa wanawake ambao waliwahi kushea kitanda na msanii huyo, Ijumaa lina mchapo kamili. Kiba alitarajiwa kufunga ndoa hiyo jana mjini Mombasa nchini Kenya kisha kufuatiwa na bonge la sherehe mjini humo huku sherehe nyingine bab’kubwa ikitarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwezi huu. MTU WA KIBA ANENA Mtu wa karibu na AliKiba, amepenyeza habari kuwa, licha ya kwamba wao wanasherehekea harusi ya mkali huyo anayetamba na Wimbo wa Seduce Me, nyuma yake kuna vilio vingi kutoka kwa wanawake ambao walitembea na Kiba kabla. “Kama unavyojua Kiba alishazaa watoto wanne, wale watoto kila mmoja ana mama yake. Sasa mama zao wanalia maana nao walikuwa wana matarajio ya kuolewa,” alisema mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina na kuongeza: BIBI HARUSI NJIA PANDA “Kimsingi wamem...

Wenger Aondoka Rasmi Arsenal

Image
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameridhia kubwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu baada ya majadiliano ya kina na uongozi wa klabu hiyo kongwe duniani. “Baada ya kutafakari kwa kina kufuatia mazungumzo na klabu yangu, u mefika wakati sasa nikae pembeni mwisho wa msimu huu, nina furaha sana kwa muda wote niliokaa hapa klabuni. “Ninawashukuru wafanyakazi wenzangu, wachezaji, wakurugenzi na mashabiki kwa kuifanya klabu hii kuwa spesho, nimeitumikia kwa miaka mingi” amesema Wenger kwenye taarifa yake rasmi leo Ijumaa. LONDON, England.

Breaking News: Masogange Afariki Dunia

Image
Video queen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde (leo Aprili 20, 2018) katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.  Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kupelekwa Muhimbili kuhifadhiwa. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu. Global Publishers imefika hospitalini hapo na kujionea umati wa watu waliokusanyika wakilia kwa uchungu kumpoteza msanii huyo. Dkt. Kihama Ngoma ameithibitishia Global Publishers na kusema taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Tayari mwili wa marehemu Masogange umehaimshwa hospitalini hapo na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, AMEN!.

Mfalme Mswati III Abadili Jina la Nchi Yake

Image
MFALME Mswati wa III wa Swaziland amebadilisha jina rasmi la taifa hilo kutoka Swaziland na kuliita Ufalme wa eSwatini (The Kingdom of Swaziland)  wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 50 na wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka 50 ya uhuru wake. Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa III kwa miaka mingi. eSwati ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 na katika ufunguzi wa bunge la nchini mwake mwaka 2014. Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki na ametawala tangu mwaka 1986.  Mswati III kwa sasa ana wake 15 akiwa anaifuata rekodi ya Baba yake aliyekuwa na wake 125. Wanaharakati wa kutetea usawa wa jinsia wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa kushangaza na unawabagua wanawake. Mswati III ametoa sababu kuu ya kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aenda...

Siwa ya Bunge yakutwa kwenye Flyover

Image
Baada ya watu wenye silaha kuvamia Bunge la Senate la Nigeria na kuiba siwa juzi, hatimaye imekutwa chini ya Barabara ya Juu ‘flyover’ Jijini Abuja baada ya kuonwa na mwananchi aliyekuwa akipita maeneo hayo. Inadaiwa watu hao waliongozwa na Mbunge Ovie Omo-Agege ambaye amefungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na tuhuma hizo. Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ya Nigeria ameeleza kuwa kitendo hicho ni uhaini na inaashiria kuwa mtuhumiwa, Omo-Agege alikuwa akijaribu kupindua moja ya mihimili ya Serikali ya Nigeria. Siwa ni ishara ya mamlaka ya Bunge hilo na Sheria haziwezi kupitishwa bila kuwepo kwa kifaa hicho. Licha ya kitendo hicho, Bunge liliendelea na kazi yake kwa kutumia Siwa ya ziada iliyokuwepo bungeni hapo ambapo kabla ya hapo Seneta wa Kaduna, Shehu Sani alivua mkanda wake na kuuweka sehemu ya Siwa hiyo. Aidha, Chama tawala, APC kimeita tukio hilo kuwa ni shambulio kwa Demokrasia ya nchi hiyo na kutaka waliohusika kukamatwa. Hadi sasa Seneta Omo-...

SHUHUDIA UKUMBI WA HARUSI YA ALIKIBA NA AMINA UNAVYOWAKA

Image
BAADA ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ kufunga ndoa na mchumba wake, Amina Khaleef Mjini Mombasa nchini Kenya leo, Aprili 19, 2018, sherehe ya harusi ya msanii huyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mombasa. Kiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu wa msanii huyo. Kiba amesema ameamua kufunga ndoa yake siku ya leo kwani siku kama hii ndiyo wazazi wake walifunga ndoa yao miaka kadhaa iliyopita.  

BABU SEYA, FAMILIA YAKE WATINGA BUNGENI – PICHA

Image
MWANAMUZIKI nguli wa dansi,  Nguza Viking ‘Babu Seya’  na watoto wake ambao ni  Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza , leo Alhamisi, Aprili 19, 2018 wametembelea  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma  baada ya kualikwa na  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile. Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai,   baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo. Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.

REKODI 3 NDOA YA KIBA!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ amefunga ndoa leo pande za Mombasa nchini Kenya, nyumbani kwa bibi harusi, Amina Khaleef, imeelezwa kuwa ndoa hiyo inatarajia kuandika rekodi ya mambo makubwa matatu. Akizungumza na Gazeti la Amani, mmoja wa mameneja wa mwanamuziki huyo, Aidan Sefu, alisema tayari wamelipwa mamilioni ya fedha na moja ya luninga ya hapa Tanzania kurekodi na kurusha live harusi hiyo.“Itakuwa kitu kikubwa sana, ni harusi ya aina yake hivyo nisingependa kuongea sana lakini watu wataona,” alisema Aidan. Kama hiyo haitoshi, Amani lilielezwa kuwa miongoni mwa rekodi zinazotarajiwa kuandikwa katika harusi hiyo ni pamoja na kukodiwa ndege maalumu ya kwenda Mombasa na kurudi Bongo. “Kutakuwa na utofauti mkubwa kwani Ali anatarajiwa kukodi ndege kumpeleka kama bwana harusi na ndege ya kumrudisha akiwa tayari na kifaa chake ili kuja kumalizia sherehe huku mwisho wa mwezi,” alisema mnyetishaji wetu. Pia mnyetishaji huyo alisema rekod...

SHUGHULI YA NDOA YA ALIKIBA IMEANZA KENYA – Picha

Image
ILE siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kushuhudia ndoa ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ hatimaye imewadia na leo Aprili 19, 2018 mkali huyo anafunga ndoa yake na mrembo Aminah Rikesh Khaleef mjini Mombasa nchini Kenya. Tayari wapenzi hao wanaofunga ndoa, Mashehe, ndugu na marafaiki wameshafika eneo ambapo ndoa hiyo inafungwa na tayari shughuli imeshaanza kama picha zinavyoonyesha. Watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo. Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine. Tazama video ushuhudie mwenyewe.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa watu 10

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 18, 2018 ameteuwa watu kumi kushika nafasi mbalimbali akiwepo Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanza April 17, 2018

Jinsi ya Kupika Pilau ya Zabibu Kavu

Image
K WENYE ukurasa huu wa Mapishi ya Amani tutaona jinsi ya kupika pilau ya zabibu kavu ambayo ni tamu sana. MAHITAJI: -Mchele -Viungo vya pilau -Mafuta ya kupikia -Nyama -Vitunguu swaumu -Vitunguu maji JINSI YA KUPIKA: Andaa mchele wako uoshe kisha weka pembeni, baada ya hapo chemsha nyama yako na yenyewe iweke pembeni, ukimaliza weka sufuria kwenye moto na mafuta, anza kukaanga vitunguu. Weka kitunguu swaumu, ukimaliza kaanga weka viungo vikaangike vizuri kisha weka mchele ukaange sana mpaka uive wakati unakaanga weka na nyama ili vikaangike kwa pamoja ukimaliza weka maji na chuvi pika pilau lako taratibu. Wengine hupendelea kuweka viazi pia ambapo huvikaanga na mafuta na viungo lakini sio lazima sana unaweza kupika pilau la nyama tu.  Pilau likishaiva sasa chukua zabibu zako kavu ziweke kwenye chakula, geuzageuza kisha funikia liache kidogo kwanza. Baadaye pakua pilau lako litakuwa tayari kwa kuliwa.

Ijue misingi ya uvumilivu katika ndoa

Image
Ni wazi kuwa migogoro kwenye uhusiano wowote ule ipo, hasa pale wenza hao wasipopeana nafasi ya kusikilizana. Kila siku narejea hii hoja kuwa, hata kwenye uhusiano wa mapenzi lazima kutakuwepo na mikwaruzano ya hapa na pale jambo la msingi ni namna ya kushughulikia misuguano hiyo bila kuibua chuki na hatimaye kuvunja uhusiano. Hata katika uhusiano wa kawaida, mikwaruzano na misuguano ni kama kukanyaga bomu, bila kuchukua tahadhari na kutegua bomu lenyewe, ukiondoa mguu mtu bomu hilo linalipuka na kuharibu kila kitu. Uvumilivu ndio jibu kubwa kwa wenza endapo itatokea kukwaruzana au kutoelewana. Endapo mwenza wako amekuudhi na kukupandisha hasira jambo la msingi kabisa ni kuhakikisha unadhibiti hasira hizo. Jaribu kuelewa kwanza tatizo kabla hasira hazijakuathiri na kukutawala. Kumbuka kuwa hasira hasara na siku zote mtu mwenye hasira huzungumza na kufanya mambo ambayo baadaye hujikuta akijilaumu. Lakini pia watalamu wa masula ya mahusiano wanasema ya kwamba siku zot...

Mbegu za Maboga Zinavyoweza Kukupa Ngozi Nzuri

Image
L EO kwenye safu yetu hii tutaona jinsi mbegu za maboga zinavyoweza kukupa ngozi nzuri na ukawa na muonekano wa kuvutia. MAHITAJI: -Kikombe kimoja cha mbegu za maboga. -Kikombe kimoja cha mafuta ya butter. -Yai moja. JINSI YA KUCHANGANYA: Chukua kikombe cha mbegu za maboga zilizosagwa, changanya na mafuta ya butter yaliyoyeyushwa. Baada ya hapo lipige yai lichanganye pia ili kuleta urahisi, tumia blenda kusagia mchanganyiko wako ukae vizuri. Ukimaliza paka mchanganyiko huo usoni acha kwa muda wa dakika kumi mpaka kumi na tano ukauke. Ukimaliza osha na maji masafi. Mchanganyiko huu ni mzuri kwa afya ya ngozi lakini pia husaidia kuondoa uchafu wote pamoja na chunusi ndogondogo

Fatma Karume aiomba radhi Serikali

Image
Rais mpya wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume ameiomba radhi serikali kwa kutoa lugha kali ambazo zilizokuwa zinaenda moja kwa moja kugusa muhimili wa Mahakama kuhusiana na mambo ambayo yanayoendelea nchini kupitia Mahakama bila ya kufuata haki za kisheria Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2018 wakati akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio kwa njia ya simu ambapo amesema zoezi la kuteua Majaji nchini liangalie zaidi taaluma za wanaoteuliwa badala ya kuwateua kwa mlengo wa kisiasa. "Mahakama ni mhimili unaojitegemea hivyo ni vema ukaheshimiwa kwa kuchagua Mahakimu wenye vigezo vya kitaaluma ambao watasimamia vema sheria badala yakuyumbishwa na siasa. Mimi nipo tayari kushirikiana na serikali kwa sababu siwezi kutengeneza bajeti lakini naweza kushirikiana nao katika kuelezea mapungufu yaliyopo", amesema Fatma. Mbali na hilo, Rais ...

Zitto Kabwe: Nipo tayari kwa lolote

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kukamatwa na polisi lakini pia yupo tayari hata kuuwawa kwa ajili ya kuisemea trilioni 1.5 ambayo CAG amesema haijatolewa maelezo imetumikaje. Zitto Kabwe amesema hayo leo April 18, 2018 baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kusema kuwa wapo viongozi wa upinzani wanasema uongo juu ya ripoti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutaka watu hao wachukuliwe hatua. Kufuatia kauli hiyo Zitto Kabwe amesema kuwa anauhakika kuwa serikali ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha matumizi ya trilioni moja na bilioni mia tano. "Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG. Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, naapa kwamba Serikali ya CCM ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni moja na bilioni mia tano. Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta...

Zuckerberg Akiri Kosa Lake Na Kuomba Radhi

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg. Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg ametoa maelezo katika Bunge la Marekani- Congress kwa mara ya kwanza Jumanne, akijibu wasiwasi ulioelezwa na wabunge juu ya kushindwa kwa mtandao wa jamii maarufu kulinda taarifa zao. Taarifa hizo za siri ni za watumiaji wanaofikia milioni 87 ulimwenguni zilizotumiwa na kampuni yenye kujishughulisha na siasa- Cambridge Analytica iliyokuwa na mafungamano na Trump. Mahojiano hayo yanaendelea Jumatano wakati Zuckerberg atakapokutana katika raundi ya pili kujibu maswali mbele ya jopo la Wabunge wa Marekani. Mkurugenzi huyo Mark Zuckerberg amekiri kuwa :”Hilo lilikuwa kosa kubwa na ni kosa langu mimi mwenyewe na naomba radhi. Nilianzisha matandao wa Facebook, niliusimamia na nina wajibika kwa kitu chochote kinachotokea.” Wachambuzi wanasema ni kosa ambalo liliruhusu kampuni ya kisiasa ya Cambridge Analytica kupata taarifa kwa kupitia programu iliyotengenezwa na k...

JPM AMBADILISHA BODIGADI WAKE, AWAPANDISHA VYEO 28

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameridhia na kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12, 2018 huku akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy ambaye amempandisha cheo na atapangiwa kazi nyingine jeshini. Aidha, Rais pia amekukubali kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murung a na kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mkeremy. Akitoa taarifa ya uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi, Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao watavalishwa vyeo vyao Ijumaa hii katika makamo makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es salaam. Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini.

ATCL Yaondolewa International Air Transport Association kwa Madeni

Image
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limeondolewa katika Mfumo wa Malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (International Air Transport Association – IATA) kutokana na kukabiliwa na madeni na sasa iimetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya Ndege ya HAHN Air ili kuuza tiketi za Air Tanzania. Akizungumza na wanahabari Mjini Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL. Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi, amesema wamelazimika kuingia kwenye makubalianao na kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma za malipo ya tiketi. “Tuna madeni, sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa ambayo yalilazimisha kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka tutakapokuwa tumelipa hayo madeni. “Kubwa zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa Shirikisho wa Mashirika ya Ndege Dunia IATA ambayo ndiyo mfumo wa uuzaji na utawanyaji wa tiketi kwa kuwa mabadilishano ya pesa au kupeleka pesa kutoka shirika moja kwenda lingine hufanyika kwa kutumia huo...

RAIS MAGUFULI AFUNGUKA ANAVYOIKUMBUKA SIKU YA MWISHO YA SOKOINE

Image
  IKIWA leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari, eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa Morogoro, Rais Dkt. John Magufuli amefunguka na kueleza alivyomfahamu kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa letu. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli amesema; “Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehemu Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho.   “Wakati tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi, unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa. “Marehem Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wa...

Lowassa asema hatapoteza muda kwenda kupimwa DNA

Image
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hamtambui mwanamke aliyejitambulisha juzi kama binti yake aliyetelekezwa na kwamba hatapoteza muda kwenda kupimwa vinasaba (DNA), kama msichana huyo alivyotaka. Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Lowassa ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema kuwa kinachofanyika kwenye zoezi hilo ni siasa. Msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma alijitokeza hadharani juzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kudai kutelekezwa na Lowassa ambaye alisema ni baba yake, kwa kuambiwa na mama yake mzazi. "Wewe unamwamini kweli huyo msichana? Angekuwa mwanangu kweli ningeshamchukua muda mrefu, kwanza wala simjui naona siasa zinaingizwa hapo," alisema. Alipoulizwa kama yuko tayari kupimwa DNA ili ukweli ujulikane, Lowassa alijibu "Kupima DNA huo ni upuuzi. Yaani nipoteze muda wangu kwenda kufanya  upuuzi huo? Siko tayari."...